Balotelli kwenye HEADLINES za rekodi ya Ubaguzi wa rangi mitandaoni England !!
Moja ya adhabu ambazo ziliwahi kumkuta mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ni uongozi wa klabu yake kumpiga faini ya pound 25,000 pamoja na adhabu ya kukosa mchezo mmoja ambao walicheza na Arsenal kwa kuwatolea maneno makali mashabiki watatu ambao walimkashifu ishu ambayo ilihusishwa na ubaguzi wa rangi.
Mara nyingi Mario Ballotelli
amekuwa akizungumziwa zaidi kwa upande mwingine.. ukorofi wake.. ishu
za kutokuelewana na kocha wake na wachezaji wenzake.. wakati mwingine
utasikia kazinguana na mashabiki.. huwa jamaa hachukulii poa kabisa
ukimhusisha na story za ubaguzi wa rangi yake.
Utafiti umefanywa na kuonesha Balotelli ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Klabu ya Liverpool ndiye
mchezaji anayeongoza kwa kupokea post nyingi zaidi kwenye mitandao ya
kijamii zinazohusu ubaguzi wa rangi katika msimu huu wa Ligi Kuu
Uingereza.
Unaambiwa kwa msimu huu pekeake amepokea
zaidi ya message 4000 huku kukiwa na nyingine zaidi ya laki moja za
ubaguzi ambazo zimewalenga wachezaji ambao wana asili ya Afrika kwenye
ligi kuu ya England.
Daniel Sturridge na Danny Welbeck pia wamefuatia kwa kupokea posts zaidi ya 1000 kila mmoja, zote zinahusu ubaguzi wa rangi.
Balotelli
ni mmoja wa mastaa wa soka ambao wanatumia sana mitandao ya kijamii,
labda hiyo nd’o sababu iliyofanya na wanaomshambulia pia kutumia njia
hiyohiyo kumtumia post hizo.
No comments:
Post a Comment