TANZANIA NAYO KUONDOA RAIA WAKE AFRIKA KUSINI
UBALOZI
wa Tanzania nchini Afrika Kusini umesema umeanza utambuzi wa Watanzania
waishio katika maeneo ya hatari nchini humo kabla ya kuanza hatua za
kuwaondoa na kuwarejesha nyumbani.
Hatua
hiyo inatokana na kushamiri kwa mashambulizi yanayofanywa na raia wa
Afrika Kusini dhidi ya raia wa kigeni ambapo hadi kufikia jana watu sita
wameuawa.
Taarifa
zilizopo hata hivyo zinasema kwamba hakuna raia wa Tanzania ambaye
ameuawa au kujeruhiwa katika vurumai hizo ambazo zimeanza Durban, Kwa-
Zulu Natal.
Mkuu wa
Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi
Kasiga, amesema kwamba Ubalozi Afrika Kusini umepeleka maofisa wake
katika mji wa Durban kuangalia hali ilivyo. Kasiga amesema kwamba Serikali imeshatoa mwongozo wa namna ya kuwaondoa raia wake nchini
Afrika Kusini.
"Utaratibu
wa kuwaondoa Watanzania upo tayari, lakini itambulike kwamba si kila
Mtanzania anayeishi Afrika Kusini ataondolewa bali wale walio katika
maeneo hatarishi.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukusogezea muda na wakati wowote hapa hapa tangakumekumechablog
No comments:
Post a Comment