Friday, April 10, 2015

MENGI MAPYA YAIBUKA KENYA SHAMBULIO LA KIGAIDI

Kingine kilichosikika kutoka Kenya kuhusu shambulio la Chuo Kikuu, kiongozi wa Serikali kahusishwa na uzembe..

img_9541Siku chache zimepita toka lilipotokea tukio la kigaidi katika Chuo cha Garissa Kenya, kwenye tukio hilo wanafunzi 148 walifariki.. kingine   kinahusu uchunguzi uliofanyika kuonesha kwamba kuna dalili za uzembe ama matumizi mabaya ya madaraka wakati wa mikakati ya kupambana na wavamizi hao.
Taarifa za kwenye vyombo vya habari Kenya zinasema ndege ambayo ilitakiwa isafirishe maafisa wa Polisi kwenda kwenye Chuo hicho kwa ajili ya kupambana na wavamizi hao ilitumiwa kwa ajili ya safari binafsi ya familia moja ambapo kuna kiongozi mmoja anahusishwa kuruhusu ndege hiyo kufanya safari hiyo wakati ambao ilitakiwa kuwapeleka maafisa hao Garissa.
Rubani amesema ndege hiyo iliondoka katika uwanja wa ndege na kuwaacha makomandoo wa RECCE wakisubiri irudi kuwachukua na kuwapeleka Garissa kuwaokoa wanafunzi.

No comments:

Post a Comment