Real Madrid wamecheza jana Elbar na hiki ndio kingine alichofanya Cristiano Ronaldo
Ligi kuu ya Hispania imeendelea tena jana usiku – huku Real Madrid na Elbar wakifungua pazia la mechi .
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameziteka tena ‘headlines’ za vyombo vya habari baada ya jana kuiongoza timu yake kupata ushindi wa magoli 3-0.
Ronaldo alifungua akaunti yake ya magoli kwa mkwaju wa adhabu ndogo katika dakika ya 21 ya mchezo huo – goli hilo limemfanya Ronaldo atimize magoli 38 katika La Liga msimu huu.
Goli hilo lilotokana na mkwaju wa adhabu ndogo ni la kwanza tangu Ronaldo alipofunga goli dhidi ya Bayern Munich katika nusu fainali ya Champions League takribani miezi 12 iliyopita.
Magoli mengine ya mchezo huo yalifungwa na Javier Hernandez Chicharito dakika ya 31 na Jesse akamalizia kazi kwa goli zuri dakika ya 83.
FC Barcelona wanaongoza ligi ya Spain walicheza na Sevilla usiku wa jana pia..
No comments:
Post a Comment