HALI ILIVYOKUWA NYUMBANI KWA GWAJIMA LEO
Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote.Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakielekea nyumbani kwa Gwajima mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
Baadhi ya waumini wakiwa mbele ya nyumba ya Gwajima.Gari la polisi likiondoka eneo la tukio.Hapa wakishangilia ushindi baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
WAKATI
taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na
polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la kumkamata askofu huyo
lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.
Polisi
hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo maeneo ya
Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo walipiga
kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa imefungwa kwa
saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya waumini wa askofu
huyo kuruhusiwa kupita.
Hata
hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na viongozi
kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri kiongozi huyo
afikie kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi ambapo
alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu ambapo taarifa
za kina kuhusu kilichojiri huko zikiwa bado hazijapatikana.
Usiwe mbali na tangakumekucha itakuhabarisha kila kinachoendelea ni hapa hapa
No comments:
Post a Comment