Kingine cha Askofu Gwajima.. Baada ya Polisi kuzunguka nyumba ishu imehamia Mahakamani..
Asubuhi ya leo imeripotiwa stori ya
Askari Polisi wakiwa na silaha kuizunguka nyumba yake, Mbezi Salasala
DAR.. waumini wake pamoja na watu wengine walikuwa pembeni pia,
kuangalia kinachoendelea.
Muda mfupi baadae imeripotiwa kwamba
Askofu huyo alienda Kituo cha Polisi Centre lakini haikuchukua muda
mrefu akatolewa na kupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu DAR..
kilichokuwa kinaendelea hapo hakuna aliyejua.
Kuna taarifa kwamba Askofu huyo
alitakiwa kuripoti Kituo Cha Polisi jana lakini hakwenda, mashuhuda
wanahisi hiyo ndio sababu iliyofanya Askari kuizunguka nyumba yake hiy
Mvutano uliopo ni kuhusu kuwasilisha
nyaraka za vitu anavyomiliki, lakini amegoma kwenda kuhojiwa mpaka
wapate barua kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ili kuwasilisha
nyaraka hizo.
Ishu ya leo asubuhi ilihusu Jeshi la
polisi kuzingira nyumba yake kwa nia ya kumtaka kujisalimisha lakini
mwenyewe alijifungia ndani na kukaidi agizo hilo, lakini habari
zilizotufikia zinaeleza mchungaji huyo tayari amefikishwa mahakama ya
Kisutu akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Mpaka sasa haijafahamika bado baada ya
kukamatwa kwake nini kinaendelea na tutaendelea kuwajuza zaidi kuhusu
hatma ya kiongozi huyo wa kanisa.
Hutopitwa na habari na niko tayari kukutumia muda na wakati wowote ni hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment