Jamaa alisinzia kwenye sehemu inayowekwa mizigo ndani ya ndege, kilichofuatia hapo ni ishu..
Ishu ilianzia pale ambapo ndege ilikuwa
imeruka kama dakika 14 hivi Uwanja wa Seattle, Marekani.. Rubani mmoja
akahisi kwamba kuna mlio wa kitu tofauti toka kwenye sehemu ambayo
inawekwa mizigo ndani ya ndege hiyo.
Marubani wa ndege hiyo ilibidi waombe
dharura kuirudisha ndege uwanjani hapo kwa kuwa walihisi sauti ya kitu
wanayoisikia toka kwenye chumba hicho cha mizigo itakuwa ni mtu.
Baada ya ndege hiyo kutua watu wa kitengo cha dharura waliingia ndani
ya ndege na kumkuta jamaa amesinzia hana hata habari na kinachoendelea.
Taarifa iliyotolewa na shirika la ndege
hiyo imesema kuwa mfanyakazi huyo alipimwa lakini hakuwa ametumia kilevi
chochote wala hakutumia dawa yoyote.. ndege hiyo aina ya Boeing 737,
iliyokuwa na abiria 170 ilikuwa imeruka kwa dakika 14 angani ikielekea
Los Angeles kabla ya kugundua kuwa kuna huyo jamaa ambaye alikuwa
ammesinzia kwenye sehemu ya mizigo ya ndege hiyo.
Hutopitwa na habari yoyote inyonifikia na nikon tayari kukutumia wakati wowotw kupitia hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment