Hivi huyu Bondia nd’o kusema alisahau akapanda na smartphone ulingoni au?
Labda tuulizane hapa mtu wangu, hivi zile bukta wanazovaaga mabondia wakiwa ulingoni zina mifuko kweli ya kuwekea vitu?
Hili swali nimejiuliza baada ya kukutana na video moja ikionesha bondia mmoja akiangusha simu wakati pambano lao likiendelea.
Pambano lilikuwa kati ya Ramon Luis Nicolas na Marvin Jones ambapo Marvin aliangusha smartphone yake raundi ya kwanza kabisa ya mchezo, referee akaiokota na kumpa jamaa.
Swali ni kwamba yani mpaka anaingia uwanjani simu hakuiona kweli?
Kaa karibu na tangakumekucha nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote.
No comments:
Post a Comment