Zikawafikia mapaparazzi PICHAZ za ndoa ya mama yake BEYONCE !!
Tina Knowles mama wa Beyonce, kibongobongo wangeongeza neno hapo, mama mkwe wa Jay Z nae kaona aachane na ubachela wa uzeeni, duh.. kafunga ndoa na actor Richard Lawson.
Wale wale mabingwa wa udaku wa mastaa duniani mapaparazzi wa TMZ.. ambao ndio waliokuwa wa kwanza pia kutoa VIDEO ya Jay Z akipigwa mateke na Solange kwenye lift, ndio waliotoa PICHAZ na video za event hiyo ya nguvu iliyofanyika katika fukwe za California.
Watu wa karibu walihudhuria party hiyo,
mapaparazzi wanasema boti ina uwezo kubeba watu 300 tu, kwa hiyo idadi
ya wageni haikuzidi namba hiyo.
Jay Z, Beyonce na mtoto wao Blue Ivy. nao walikuwa sehemu ya party hiyo.
Tina na mzee Mathew Knowles walipeana talaka mwaka 2009, hapo ilikuwa miaka 30 tangu wafunge ndoa yao.. halafu uhusiano wa Richard na Tina ukaanza 2013.
Unfortunately your browser does not support IFrames.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment