Monday, April 13, 2015

NYUMBA 1O KALI ZA KUSHANGAA DUNIANI, HIZI HAPA

Hizi nazo ziko kwenye list ya nyumba kumi kali, ila zilivyokaa ni ishu yani..

The-Upside-Down-House-Poland
Basi mtu wako nikakutana na bonge la HEADLINE mtandaoni yani.. “10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHAZ ya hizo nyumba kali huko DUNIANI.
Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe mtu wangu  uzione labda iko itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.
Antilia-India
Unaambiwa hii inaitwa Antilia, iko India. Nayo iko kwenye list mtu wangu.
Bio-Climatic-Solar-House-France
Inaitwa Bio Climatic Solar House, iko Ufaransa. Ilivyokaa kaa ni kama sio mjengo wa kuishi yani.
Boeing-727-House-Costa-Rica
Boeing 727 House, hii sio mara ya kwanza kuiona mtu wangu. Haikunishtua nilipoiona tena.
Bubble-House-France
Ilinipa tabu kujua nini kinaendelea hapa. Naona kama mapango mapango tu hivi, lakini nd’o mjengo huo yani. Bubble House, iko Ufaransa.
Crazy-House-Vietnam
Duuh, jina lake tu ni balaa yani. Inaitwa Crazy House, iko Vietnam.
Crocodile-House-Ivory-Coast
Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwa Crocodile House.
Dar-al-Hajar-Yemen
Hii nayo ni ghorofa ya aina yake yani. Dar-al-Hajar, iko Yemen huko.
Shoe-House-South-Africa
Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwa Shoe House, iko South Africa.
The-Toilet-House-South-Korea
Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.
toilet
Hiyo Toilet House ya Korea inavyoonekana kwa juu.

.
Kama imepinduka hivi.. kumbe hapo nd’o iko sawa. Hujaipenda hii mtu wangu? Wenyewe wanaiita The Upside Down House, iko Poland.
Nitafurahi kuona umendikia nyumba ipi imekuvutia zaidi kati ya hizo mtu wangu !!

No comments:

Post a Comment