Wednesday, April 15, 2015

MUHEZA WATAKA NAKALA YA KATIBA PENDEKEZWA, WATISHIA KUISUSIA

Tangakumekuchablog

Muheza,WAKAZI Wilayani Muheza Mkoani Tanga, wameitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, kuisambaza Katiba Pendekezwa na kuwapa muda wananchi kuisoma kwa kina kabla ya kuipigia kura.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara   ulioitishwa na Kituo cha Sheria na Haki za Bianadamu (LHRC) uwanja wa soko la Tanganyika na kusema kuwa Tume isambaze kila kaya  Katiba Pendelezwa na kuweza kusomwa kwa kituo.

Walisema kufanya hivyo kutawapa nafasi wananchi siku ya kuipigia kura kujitokeza kwa wingi kwa kutambua walichokisoma na kusema kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kuhakikisha kila kaya imepata Katiba Pendekezwa.

“Unajua wengi tunasikia kuwa kuna siku ya kuipigia kura katiba pendekezwa ila sie hatuijui wala kuiona-----itatuwia vigumu kupiga kura kitu ambacho hatukijui” alisema Michael Mhina

“Ili kuliwezesha jambo hili ambalo niko na maslahi na wananchi ni vyema tume ya mabadiliko ya katiba mpya kuisambaza katiba pendekezwa kila kaya na kuwapa nafasi wananchi kuisoma” alisema

Awali akiwahutubia wananchi,Mratibu wa zoezi la kutoa elimu ya uraia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Stanley Humbo, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa kuipigia kura Katiba Pendekezwa.

Amesema ni haki ya kila mtu kuchukua maamuzi sahihi ya kuipigia kura Katiba Pendekezwa kwani maoni yake ndio ambayo yatazaa  kupatikana kwa Katiba Mpya ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikilalamikiwa kwa baadhi ya mambo.

Amesema maoni hayo  yatakayowezesha  kupatikana Katiba Mpya ambayo kwa muda mrefu wananchi walikuwa wanaisubiria ikiwa na pamoja na kuondosha manung’uniko kwa baadhi ya mambo yaliyomo.

“Ndugu zangu wa Muheza ni wajibu wa kila mmoja kujitokeza siku ya kuipigia kura katiba pendekezwa kwani iko na maslahi na wananchi na Taifa kwa ujumla” alisema Humbo

Alisema Katiba hiyo Pendekezwa itagawiwa na kila mmoja kuisoma kwa nafasi na hivyo kuwataka kujitokeza kwa wingi siku ya kuipigia kura na kuweza kupata Katiba mpya ambayo itatuongoza kwa miaka mingi.

                                               Mwisho



 Mratibu wa zoezi la kutoa elimu Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Stanley Humbo akizungumza na wakazi wa Muheza Tanga juu ya kujitokeza siku ya kuipigia kura Katiba Pendekezwa mkutano uliofanyika uwanja wa soko la Tanganyika

Wakazi wa Muheza Tanga wakisikiliza elimu ya elimu ya upigaji kura Katiba Pendekezwa iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mkutano uliofanyika viwanja vya soko la Tanganyika

 Wakazi wa Muheza Tanga wakisikiliza elimu ya upigaji kura Katiba Pendekezwa iliyokuwa ikitolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu  (LHRC) mkutano uliofanyika uwanja wa soko la Tanganyika

No comments:

Post a Comment