Hizi ndio nchi zilizoongoza kwa kunyonga watu mwaka 2014, Afrika nani anaongoza?
Unaambiwa
idadi ya watu walionyongwa imekua na tofauti katika mwaka 2013 na 2014
kwenye nchi mbalimbali duniani ambapo mwaka 2013 watu waliohukumiwa
kunyongwa ni 778 kote duniani tofauti na mwaka 2014 ambapo walionyongwa ni 607 imeshuka kwa ongezeko la sawa na asilimia 22.
Sawa idadi ya walionyongwa imeshuka lakini
taarifa ikufikie tu kwamba idadi ya waliohukumiwa kunyongwa kwa mwaka
2014 ni 2,466 ni idadi ambayo imepanda kwa asilimia 28 ukilinganisha na
mwaka 2013.
Kwenye hii picha hapa chini ndio unapata picha kamili nchi zilizoongoza kwa kunyonga watu mwaka 2014.
Nchi
iliyoshika namba 1 ni Iran kwa kunyonga watu 289, ya pili ni Saudi
Arabia kwa kunyonga watu 90, ya tatu ni Iraq ambayo ilinyonga watu 61,
ya nne ni Marekani iliyonyonga watu 35 na Yemen ndio wamechukua namba 5
kwa kunyonga watu 22.
Nchi ambazo
zina idadi ndogo ya watu walionyongwa ni Singapore iliyonyonga watu
wawili, Gaza/West Bank watu wawili, Japan watu watatu.
Kwenye nchi
za Afrika zilizoongoza kwa kunyonga watu mwaka 2014 ni Sudan 23, Egypt
ndio imeshika namba 2 kwa kunyonga watu 15, Somalia 14 wamechukua namba
tatu na wa mwisho kwenye hii list Equatorial Guinea walionyonga watu 9.
Ninazo zote kubwa za kila siku na ukijiunga na mimi kwenye www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment