Uamuzi huu wa Raheem Sterling unaichanganya Liverpool…
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Raheem Sterling amewachanganya
mashabiki na viongozi wa timu hiyo baada ya wawakilishi wake kusema
kuwa mchezaji huyo hatasaini mkataba mpya hadi hapo msimu
utakapomalizika.
Ripoti zaidi nchini England zinasema kuwa Raheem amegoma kusaini mkataba mpya baada ya kutoridhishwa na kiwango cha fedha ambacho Liverpool imeahidi kumlipa kwa wiki ambapo inadaiwa kuwa klabu hii imetoa ofa ya paundi 100,000/= kwa wiki.
Taarifa kadhaa huko England na barani ulaya kwa jumla zimeendelea kumhusisha Sterling na mpango wa kuihama klabu yake ambayo ilimpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 18 tu.
Real Madrid na Arsenal
zimekuwa zikitajwa kuwa na mipango ya kumsajili kiungo huyo ambaye hadi
sasa ametokea kuwa sehemu muhimu katika mipango ya kocha Brendan Rodgers.
Kitendo cha Sterling kugoma
kusaini mkataba mpya kimepokewa kwa hisia hasi miongoni mwa mashabiki
wa klabu hiyo na wachezaji wa zamani ambao wamejenga dhana ya kuwa
wachezaji wa kizazi cha sasa wanaendeshwa na tamaa ya fedha na si
mapenzi kwa timu zao na mchezo wa soka pamoja na heshima kwa mashabiki
na historia ya klabu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment