Uchambuzi huu unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya Taifa na wale wanaojiendeleza. Kituo pia kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
NIPASHE
Serikali imepunguza idadi ya masomo
kutoka saba hadi matatu kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la pili
lengo likiwa ni kuboresha mfumo wa elimu nchini.
Masomo ambayo wanafunzi hao watatakiwa kuyasoma ni Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Naibu Waziri wa elimu Kassim Majaliwa alisema alisema hayo wakayi akifungua mafunzo ya mtaala mpya ya walimu wa darasa la kwanza na la pili mjini Dodoma.
Alisema mabadiliko hayo ni kutokana na sera mpya ya elimu iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Kikwete.
“Zamani
wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili walikuwa wanasoma masomo saba,
lakini katika sera hii mpya yamepungua na kubaki matatu” MAJALIWA.
Alisema katika sera hiyo mpya mwanafunzi
atakayeshindwa kufaulu katika masomo hayo matatu hataruhusiwa kuendelea
na darala la tatu.
Alisema vitabuvoye vitakavyotumika kufundishia shule za msingi na Sekondari vitakuwa vya aina moja kila darasa.
NIPASHE
Serikali imetangaza viwango vipya vya
nauli za mabasi zitakazoanza kutumika kuanzia Aprili 30, mwaka huu, huku
nauli za magari hayo yanayokwenda mikoani zikishushwa na zile za
daladala zinazotoa huduma maeneo ya mijini zikiendelea kubaki kama
zilivyo.
Nauli hizo mpya zilitangazwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini Nchini (SUMATRA), Gilliard Ngewe.
Alisema punguzo la nauli hizo ni asilimia 7.8 kwa daraja la kawaida la chini na asilimia 5.81 daraja la kati.
Ngewe alisema viwango hivyo vimebadilika kutokana na kushuka kwa kwa bei ya mafuta mwishoni mwa mwaka jana.
Alisema kutokana na kushuka kwa bei ya
mafuta, Sumatra imekuwa ikipokea wito wa kupitia upya viwango vya juu
vya nauli vilivyowekwa na mamlaka hiyo Aprili, 2013.
Pia alisema wamefanya mabadiliko hayo
baada ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau na wamiliki wa usafirishaji
katika mikutano mbalimbali iliyofanyika jijini Mwanza, Dar es Salaam na
Arusha.
Alisema Machi 9, mwaka huu, Baraza la
Ushauri la Watumiaji wa Huduma Zinazodhibitiwa na Sumatra (SCCC)
liliwasilisha kwa Sumatra maombi ya kushusha nauli za mabasi ya masafa
marefu na mijini.
Ngewe alisema katika maombi hayo baraza
liliainisha sababu za kuomba punguzo hilo kuwa ni kushuka kwa bei za
mafuta na kodi ya forodha kwa mabasi mapya kutoka asilimia 25 hadi 10.
NIPASHE
Wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na
wananchi katika maeneo mengi nchini, wamepinga vikali tishio la Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, la kuzifuta
taasisi za kijamii na kidini na kueleza kuwa amekurupuka, hakushauriwa
na kushindwa kufuata misingi ya demokrasia na Katiba ya nchi.
Wakizungumza katika maeneo mbalimbali
nchini jana, wadau hao walidai kuwa, kufanya hivyo ni kusababisha vurugu
na udikteta mkubwa kwa nchi inayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora
na demokrasia.
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Askofu wa Jimbo la Rulenge, mkoani Kagera, Severin Niwemugizi,
alisema amelipokea tamko hilo kama matamshi ya watu ambao hawajakomaa
kisiasa, wasio tayari kupokea maoni ya wengine tofauti na yao na kwamba
halina haki bali limejaa woga.
“Katika
nchi ya demokrasia yenye viongozi wa namna hii hawana tofauti na
madikteta, ukianza kutishia wenzako kuwa ukisema maneno nisiyoyapenda
nakufuta huo ni udikteta,” alisema na kuongeza:
“Sheria
ya kura ya maoni inasema kutakuwa na makundi ya ndiyo na hapana,
najiuliza ni kundi lipi la pande hizo, kwanini wawepo wanaozuiwa
wasihamasishe watu kusema hapana kama taasisi za serikali zinazoruhusiwa
kuhamasisha ndiyo?” alihoji.
Baadhi ya asasi za kijamii na watu
binafsi mkoani Arusha, walisema tishio hilo ni udikteta ambao ni aibu
kutolewa na viongozi katika nchi inayothamini demokrasia na kwamba
inapaswa kukemewa kwa vile ina lengo la kupora uhuru wa kujieleza ambao
upo kikatiba.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la
kiserikali la Utetezi wa Haki za Wafugaji, Warina Asali na Waokota
Matunda (Pingo’s Forum), Edward Porokwa, alisema kauli ya Waziri Chikawe
ni tishio kubwa linalowanyima uhuru wa kujieleza.
Mkurugenzi wa asasi ya Grassroot Youth
Development Organisation (GYDO), Henry Cigwasi, alishauri matamko
mengine ya viongozi wa serikali yatolewe baada ya kufanyiwa utafiti.
Alisema maisha yote ya binadamu ni
siasa, kila kitu anachofanya ni siasa, hivyo hawawezi kuacha kuzungumzia
au kutoa elimu ya uraia bila kuzungumzia masuala muhimu yanayohusu
maisha yao.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana,
alisema inaonyesha waziri alikurupuka bila kushauriana na kwamba siyo
kauli inayopaswa kutolewa kwa umma katika zama hizi za demokrasia na
siasa huria.
“Amekosea,
ninachojua serikali haiwezi kufuta Katoliki au KKKT, utajiridhisha
umewafutia, lakini dini itaendelea kuwapo, askofu hawezi kufuta
ukatoliki wangu, hayo yanatokea kwenye mataifa yenye udikteta pekee,” .
Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, alisema: “Jukumu
kubwa la serikali yoyote ni katika ‘law and order’ na ‘stability’,
lakini serikali ya kidemokrasia haitumii mabavu bali unaweza kujenga
amani na utulivu kwenye nchi kwa kujadiliana,” .
MWANANCHI
Hoja za kisheria alizowasilisha Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuhusu kutakiwa kuwasilisha nyaraka 10 za utajiri na usajili wa kanisa lake polisi zimezaa matunda.
Sasa, agizo la Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam la kumtaka Askofu Gwajima kuwasilisha nyaraka hizo leo
limesitishwa kusubiri utatuzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
au Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka.
Wakili John Mallya
anayemtetea Askofu Gwajima alilieleza gazeti hili jana usiku kuwa baada
ya makubaliano na polisi mteja wake leo hatafika Kituo Kikuu cha Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kama ilivyokuwa imepangwa mpaka hoja hizo
za kisheria zitakapotolewa uamuzi.
Alhamisi iliyopita, polisi ilimtaka
Gwajima kuwasilisha vielelezo hivyo, lakini hatua hiyo ilipingwa na
kiongozi huyo akieleza kuwa hatapeleka nyaraka yoyote iwapo jeshi hilo
halitajibu barua aliyoliandikia kutaka liombe vitu hivyo kwa maandishi.
Nyaraka zilizotakiwa kuwasilishwa polisi
ni hati ya usajili wa kanisa, namba ya usajili, majina ya Baraza la
Wadhamini, idadi ya makanisa anayohudumia na nyaraka za helikopta ya
kanisa.
Nyaraka nyingine ni; muundo wa uongozi
wa kanisa, waraka wa maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba
na mali za kanisa, nyaraka kuonyesha taarifa za hesabu kutoka kwa
Msajili wa Vyama vya Hiari na kuambatana na mtu anayepiga picha za video
kanisani hapo.
Katika barua yake kwa polisi, Wakili Mallya alisema: “Tunaiomba
Polisi kumwandikia rasmi mteja wetu kimaandishi nyaraka mnazozihitaji
na vifungu vya sheria vinavyotumika na polisi kutaka nyaraka hizo…
tutashukuru kupata hati hiyo.”
Mapema alipoulizwa kuhusu kitakachotokea leo, Kamanda Kova alisema: “Suala
la Mchungaji Gwajima kwenda na vielelezo alivyoagizwa na Polisi siwezi
kulizungumzia hadi hapo itakapotokea hakuja navyo ndipo nitakapotoa
tamko langu la mwisho.
MWANANCHI
Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo, juzi alifanya tukio la aina yake pale alipomtangaza Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael kuwa ndiye atakayerithi mikoba yake.
Tangazo hilo sasa linavunja minong’ono
iliyokuwa imezagaa kwamba Ndesamburo hatagombea tena nafasi hiyo katika
uchaguzi mkuu ujao, baada ya kuliwakilisha jimbo hilo kwa miaka 15
kuanzia 2000.
Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa Kilimanjaro alimtangaza Michael katika mkutano wa hadhara
uliofanyika viwanja vya Manyema kuwa ndiye anatamani awe mrithi wake.
“Niwatafutieni mbunge nisiwatafutie? Niwatafutieni mrithi wangu niache? Nimtaje nisimtaje?”, hayo ndiyo maneno aliyoyatumia Ndesamburo kuwauliza wananchi kama amtaje mrithi wake au la.
“Mtaniunga
mkono kwamba nitakayemtaja ndiye mtakayemsaidia? Jaffar njoo hapa bwana
(akimwita Meya). Sasa nawaambia wakati ukifika ndio huyu
nitakayemfanyia kampeni,” Ndesamburo.
Huku akiwa amemnyanyua mkono, Ndesamburo alisema muda ukifika atamleta Michael mbele ya wananchi ili wamfanyie kampeni.
“Nimefanya hivi kwa ajili ya kuondoa majungu, kwa ajili ya kuondoa makundi na kwa ajili ya kujenga umoja wa chama chetu,” alisema huku akimsifia kuwa ni mtu msafi na anayewajibika kwa wananchi.
Hata hivyo, katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema alipoulizwa jana kuhusu uamuzi huo wa Ndesamburo alisema haikuwa sahihi kumtangaza mrithi akisema ni kinyume cha Katiba yao.
“Ninakubali
maoni yake binafsi kama binadamu, lakini kama mwenyekiti wa mkoa
haikuwa sahihi kwa sababu hiyo ni kinyume cha Katiba. Akifanya hivyo
anaminya demokrasia ndani ya chama,”.
MTANZANIA
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro,
linawashikilia watu 10 waliokamatwa msikitini wakiwa na vifaa
mbalimbali, ikiwamo milipuko 30, sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na bendera nyeusi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonald Paul
alisema tukio hilo lilitokea Aprili 14, mwaka huu saa 3.30 usiku katika
Kitongoji cha Nyandero, Tarafa ya Kidadu wilayani Kilombero.
Kamanda Paul alisema watu hao
walikamatwa katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu, ambapo mmoja kati ya
watu hao ambaye anadaiwa kuwa mwenyeji wa kundi hilo, aliuawa na
wananchi kwa kuchomwa moto.
Kamanda Paul alimtaja mtu huyo kuwa ni Hamad Makwendo Mkazi wa Manyasini Ruaha wilayani Kilombero.
Alisema siku ya tukio, polisi walipata
taarifa za watu wanaojihusisha na uhalifu na kuanza kufuatilia tukio
hilo na kwamba baada ya kufika eneo la tukio walikuta watu hao
wameondoka.
“Askari wetu walipofika pale walikuta watuhumiwa wote wameondoka kwa kutumia usafiri wa bajaji mbili,” Kamanda Paul.
Alisema wakati wakiendelea na ufutiliaji, walikutana na bajaji moja ikiwa na abiria mmoja ambapo walilazimika kuisimamisha.
Alisema baada ya kuisimamisha bajaji hiyo, mtu mmoja aliruka na kuanza kukimbia ndipo askari mwenye namba F.3323 Koplo Nasoro alianza kumkimbiza na alipomkaribia mtuhumiwa huyo alichomoa jambia na kumkata askari huyo shingoni.
Alisema askari mwingine mwenye namba
E9245 Koplo Chomola ambaye alikuwa nyuma, alifanikiwa kumpiga risasi ya
mguu mtuhumiwa huyo na kuanguka chini.
Alisema baada ya kuanguka, wananchi wa eneo hilo tayari walikuwa wamefika na kuanza kumshambulia na baadae kumchoma moto.
Hata hivyo, Kamanda Paul alisema
iliwalazimu kuongeza askari wengine ili kuwasaka watu wengine ambapo
walipata taarifa za uwepo wa watu msikitini humo.
Alisema polisi walipofika katika msikiti
huo, waliomba viongozi wa msikiti kuwatoa watu wote waliokuwamo
msikitini ili kuwabaini wahalifu kwa sababu wanatiliwa shaka.
Alisema waumini wote walitakiwa kutoka
nje ya msikiti wakiwa na mabegi yao, ambapo polisi waliendesha ukaguzi
na kufanikiwa kuwakamata watu kumi.
Kwa mujibu wa Kamanda Paul, vitu
vilivyokutwa katika mabegi hayo ni pamoja na milipuko 30 na bendera
nyeusi iliyoandikwa maneno ya Kiarabu na Kiswahili yenye maana ya Mungu
Mmoja.
Vifaa vingine walivyokutwa navyo ni
nyaya za umeme, majambia , bisibisi, vifaa vya kujikinga puani (maski),
sare moja ya Jeshi la Wananchi na nyingine ambazo hazikujulikana kutoka
nchi gani.
Vifaa vingine walivyokutwa navyo ni misumeno, spana ya kufungulia mabomba, madaftari na vitabu mbalimbali vikiwemo vya risiti.
Alisema mbali na vitu hivyo, marehemu
alikutwa na risasi sita, kati ya hizo tano ni za Sub Machine Gun (SMG)
na moja ni ya bunduki ya Mark IV.
MTANZANIA
Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo),
kimesema kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa
lengo la kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya
wananchi.
Kutokana na hali hiyo, kimewahakikishia
Watanzania kuwa ujio wa chama hicho ni wa kuleta mageuzi ya kweli kwa
taifa badala ya porojo kama vyama vingine vinavyofanya.
Akihutubia wananchi jana katika mkutano
wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ukombozi, mjini
hapa, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kuwa hivi sasa
Taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia
ya kufanikisha malengo ya kukitoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), madarakani.
Alisema kutokana na hali hiyo, ni lazima
Taifa lijengwe upya kwa matumaini, ikiwamo kuhakikisha vyama vinakuwa
na ushirikiano wa dhati utakaoleta mageuzi ya kimfumo na uchumi kwa
Watanzania wote.
“ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi
zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu,
Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba.
Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na si ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
MTANZANIA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema kumekuwapo na mafanikio katika vita dhidi ya majangili kwenye hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita, majangili walivamia kwa kasi na kuwaua wanyamapori wakiwamo
tembo na faru, hatua ambayo iliibua tishio la kutoweka kwa baadhi ya
wanyamapori.
Juzi Waziri Nyalandu alitangaza
kukamatwa kwa silaha za kivita zikiwamo bunduki za AK 47 na SMG katika
Pori la Akiba la Rungwa lililopo katika wilaya za Manyoni na Chunya.
Silaha hizo zimekamatwa kutoka mikononi
mwa majangili, ambapo katika msako huo, majangili 10 yalikamatwa kabla
ya kukamilisha mipango ya kuua tembo.
Akizungumza baada ya kukagua silaha
zilizokamatwa, Waziri Nyalandu alisema Serikali kamwe haitarudi nyuma
hadi majangili wasalimu amri.
Alisema kukamatwa kwa shehena ya silaha hizo zikiwamo na kivita ni salamu kwa majangili.
Nyalandu alisema hakuna jangili ambaye atakuwa salama iwapo hataweka silaha chini na kuwa Serikali lazima ishinde.
Nyalandu alisema hakuna jangili ambaye atakuwa salama iwapo hataweka silaha chini na kuwa Serikali lazima ishinde.
Kaimu Meneja wa Pori la Rungwa, Kwaslema
Male, alisema silaha hizo zimekamatwa katika kipindi cha kuanzia
Januari 2012 hadi Aprili, mwaka huu, huku idadi kubwa zikiwa zimekamatwa
mwanzoni mwa mwaka huu.
HABARILEO
Serikali ya Tanzania inatarajia kufungua ubalozi nchini Kuwait kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha wa 2014/2015.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alipokutana na Shehe Sabah Al-Khalid Al-Sabah, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait, juzi jijini Kuwait City, Kuwait.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao
wawili walisifu ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili, ambao ni wa
kindugu na unalenga kuwanufaisha wananchi wa nchi hizi.
“Kwa
kufungua ofisi za Ubalozi, Kuwait ushirikiano huu wa kidugu utaongezeka
kwenye nyanja zote muhimu na utazaa matunda yatakayo wanufaisha watu
wetu, kwa nchi hizi mbili,” Membe.
Kwa upande wa Kuwait, Serikali yao ilifungua ubalozi nchini Tanzania Februari mwaka huu na Jassem Ibrahim Al Najem ndiye Balozi wake wa kwanza nchini Tanzania, mwenye makazi yake Jijini Dar es salaam.
Kwa sasa Tanzania inawakilishwa nchini Kuwait kupitia Ubalozi wake uliopo Riyadh, Saudi Arabia.
Katika mkutano huo, Sabah Al- Khalid Al
Sabah alisifu jitihada za Tanzania za kulinda na kuleta amani barani
Afrika hususan kwenye maeneo yenye migogoro.
Alisema Serikali yake itaendelea
kushirikiana na Tanzania, sio tu kwenye maeneo muhimu ya maendeleo,
lakini pia hata kwenye ulinzi wa amani, kwani ndio changamoto kubwa
inayoikabili dunia kwa sasa.
Kuhusu misaada barani Afrika, viongozi
hao walijadili suala la uratibu wa misaada mbalimbali ya Serikali ya
Kuwait, ambapo waliangalia uwezekano wa kuanzisha kituo maalum nchini
Tanzania kwa ajili ya kusimamia shughuli za uratibu wa misaada hiyo.
JAMBOLEO
Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoani
Dodoma imewahukumu mume na mke kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la
kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin.
Watuhumiwa hao ni Halid na Marium Mwanzalima wakazi wa eneo la Hazina Wilani humo.
Watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Juni mwaka jana eneo la Hazina kinyume cha sheria.
Kabla ya kutolewa hukumu watuhumiwa hao
walipewa muda wa kujitetea ndipo mume akaomba mahakama impunguzie adhabu
kwa kuwa yeye ni mlemavu wa miguu hivyo hawezi kufanya kazi nzito.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment