Wednesday, April 15, 2015

UZUSHI WA KIFO CHA MSANII , HUSSEIN MACHOZI

Kuhusu zilizosambaa juu ya kifo cha Hussein Machozi, makubwa mengine yametokea nyumbani kwao Singida.

Hussein 1Ni jioni ya Jumatano ya April 15 2015 jana taarifa  zilizoenea kwamba msanii wa bongofleva Hussein Machozi amefariki kwenye ajali iliyohusisha gari la mizigo na gari dogo Dodoma.

Ajali 1
Katika picha zilizosambaa na kumuhusisha Hussein Machozi, hii ni mojawapo.
Hussein alipatikana na kuzungumza hivi
Nilijiandaa hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana, msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipo Dar es salaam
Kumbe baada ya taarifa za kifo kusambaa na kuwafikia Mama yake mzazi pamoja na dada yake ambao walipiga simu yake na haikupokelewa kwa muda mrefu, wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.
Ajali 2Sasa hivi Hussein inabidi alazimike kusafiri mpaka kwao Singida Manyoni ili kuwahakikishia ndugu zake kwamba yuko hai manake aliongea kwenye simu ya kaka yake na kumpa Dada simu baada ya kuzinduka lakini dada hajaamini, kasema anafichwa tu lakini ni kweli Hussein kafariki.

No comments:

Post a Comment