Wednesday, April 15, 2015

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Msichana kamkataa mpenzi wake, eti nd’o akataka kumuua?

breakup_7Leo Tena huwa inakuwa na story nyingi sana zinazotokana na mkusanyiko wa matukio ya kila siku mtaani..  leo ni ishu ya binti mmoja maeneo ya Msasani Dar, ambaye aliingia kwenye ugomvi na mpenzi wake.
Msichana huyo amesema mpenzi wake huyo alimfuata nyumbani kwake na kumnywesha kwa nguvu maji ya betri kwa lengo la kumuua.
Dada wa msichana huyo amesema alitumiwa message na mwanaume huyo kwa kutumia simu ya mdogo wake, akimtaarifu kuwa hajui kama mdogo wake ni mzima au amefariki, dada huyo akaamua kufuatilia na kukuta mdogo wake amepelekwa Hospitali ya Mwananyamala huku akiwa kwenye hali mbaya.
Chanzo cha ugomvi wanasema ni ishu ya msichana huyo kumkataa mwanaume baada ya kugundua kuwa ana mke.. siku ya tukio mwanaume huyo alimfuata nyumbani kwake, akamlazimisha kuingia ndani na kuaanza kumkaba huku akimnywesha maji ya betri.
Baadae mwanaume huyo alikimbia lakini bado ameendelea kuwatumia ujumbe wa kuwataarifu kuwa atahakikisha anamuua msichana huyo na yeye atajiua.

No comments:

Post a Comment