Muuguzi alicheki njia ya kurahisisha kazi yake, hiki alichoamua ni sawa kweli?
Zamani
kulikuwa na misemo ambayo ilikuwa ikitumiwa sana, utasikia kazi fu’lani
ni wito.. ilikuwa kawaida yani, ukikutana na Mwalimu utaambiwa ualimu ni
wito.. Daktari nae utasikia udaktari ni wito.. siku hizi sio maneno
ambayo yanasikika sana.
Nimekusogezea hii story toka Jamhuri ya
Czech, muuguzi mmoja kafikishwa Mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha
maisha.. kesi iliyofanywa ashitakiwe imenishtua kiukweli.
Unajua ikitokea mtu unaumwa au
hajisikii vizuri unaenda zako Hospitali ili kucheki kama una tatizo ili
utibiwe.. lakini kitendo cha huyu muuguzi kinaweza kukushtua na wewe
pia, yeye kaamua kuyakatisha maisha ya wagonjwa, kisa alikuwa ameelemewa
na kazi kwa hiyo akaona azidishe potassium kwa wagonjwa ili kupunguza
mzigo wa kazi.
Vera Maresova ambaye umri wake ni miaka 50 aliyekuwa akifanya kazi katika hospitali moja iliyoko Rumburk
ambapo amefanya kazi kwa miaka minne aliamua kuwachoma sindano zenye
Potassium wagonjwa ambao ni wanawake watano na mwanaume mmoja kwa lengo
la kuwaua.
Yani eti wagonjwa wanaohitaji huduma yake walikuwa wengi, akaamua kuwapunguza ili wabaki wachache aweze kuwahudumia.
Ripoti ya Uchunguzi wa Polisi inaonesha Maresova
aliwachoma sindano zenye sumu hiyo wagonjwa hao kwa nyakati tofauti
kati ya mwaka 2010 na 2014, kesi imeisha na kahukumiwa kifungo cha
maisha jela.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment