Rais wa FIFA Sepp Blatter anavyofananishwa na watu hawa mashuhuri duniani!!
Blatter
ameendelea kuonekana huenda akatetea kiti chake kwa mara nyingine baada
ya wanachama kumi wa Shirikisho la soka Amerika ya Kaskazini, Amerika
ya Kati na Muungano wa visiwa vya Carribbean (CONCACAF) kumuunga mkono kiongozi huyo katika uchaguzi mkuu.

Kitendo
cha wanachama hao kufanya hivyo kimemfanya Blatter kufafanishwa na watu
mashuhuri duniani walioweka historia na kujipatia umaarufu mkubwa kama
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela, Winston Churchill, Abraham Lincoln na Martin Luther King.
Rais wa CONCACAF, Jeffrey Webb alisema wanachama wake wanaendelea kumuunga mkono Blatter.
Wengine wanaowania Urais wa FIFA ni pamoja na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ureno Luis Figo, Mholanzi Michael van Praag, na Ali Bin Al Hussein.
Hutopitwa na habari yoyote inayotokea na kuwa karibu nami hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment