Trafiki na dereva wa bodaboda wamepata ajali na kufariki.. kisa ni ishu ya rushwa?
Baada ya mtu huyo kugoma kutoa rushwa
ambayo Afisa huyo aliitaja, alimtoroka na kukimbia.. Askari
akamsimamisha jamaa wa bodaboda ili wamkimbize, safari yao haikufika
mbali.. walipata ajali hiyo kwa kugongana na gari ndogo.
“Kuna
mtu alikuwa amemshika akiwa amebeba begi sasa huyo mtu alimpatia elfu
moja yule Askari akakataa.. alipokataa huyo jamaa akachomoka akavuka
akaingia kwenye matatu iliyokuwa imetelemka hivi”–alisema mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Ajali hiyo ilifanya dereva wa pikipiki na Askari huyo kufariki eneo la tukio.
Kutokana na Sheria za nchi hiyo Polisi haruhusiwi kupanda gari lolote wala pikipiki anapomkamata mtu.
No comments:
Post a Comment