Uchambuzi huu wa magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita wanaofanya mitihani ya Taifa na wale ambao wanajiendeleza. Kituo pia kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer na kutoa Sataficate. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246
JAMBO LEO
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe
amesema misukosuko aliyoipata katika Uliongo wa siasa kwa muda wa mwaka
mmoja uliopita umemfanya awe na ujasiri na moyo wa chuma.
Zitto
amesema ujasiri wake ulianza mwaka 2007 wakati wa sakata la BUZWAGI
japo hakuungwa mkono na Wabunge wengi lakini alifanya kila jitihada
kuhakikisha Watanzania wanajua uovu wa viongozi wao.
Zitto amesema hatojibu madai
anayozushiwa kwamba amejiunga ACT ili kuwaandalia njia viongozi wengine
ambao wanataka kugombea Urais.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira amesema ni jambo la kusikitisha kuona watu wanashindwa kusimama na hoja za kimaendeleo badala yake wanakaa kusikiliza uzushi.
NIPASHE
Mwalimu wa chekechea Mollen Calleb,
aliyesimama mahakamani kwa kujifanya mzazi wa mtoto wa miaka miwili
aliyejeruhiwa kwa kupigwa na mlezi wa shule ya chekechea ya Nelca Day,
amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuidanganya
mahakama.
Mwalimu huyo anatuhumiwa kuidanganya
mahakama na kusababisha kesi hiyo ya kujeruhi kufutwa bila mlalamikaji
kuwepo katika Mahakama ya Mwanzo Ilemela, Mwanza, ilifuta kesi ya
kujeruhiwa mwanafunzi, inayomkabili mlezi wa shule ya chekechea ya Nelca
Day Care, Siwema Bujota anayedaiwa kumpiga mtoto huyo na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili.
Bujota aliyekuwa na
dhamana ya kulea watoto shuleni hapo, alimjeruhi mwanafunzi wa miaka
miwili (jina limehifadhiwa), kwa kumchapa viboko kwa madai kuwa
alijisaidia haja kubwa shuleni.
Baada ya kesi hiyo kufikishwa mahakamani, mwalimu wa shule hiyo, Calleb
alikwenda mahakamani na kujitambulisha kwamba yeye ndiye mlalamikaji
wa kesi hiyo na kuiomba mahakama kuifuta kwa madai kuwa hakuwa na nia ya
kuendelea na mashitaka na kwamba watamalizana nje ya mahakama ambapo
Mahakama hiyo ilifuta kesi bila kujua kwamba aliyesimama mahakamani sio
mlalamikaji halali.
Mlalamkaji katika kesi hiyo alikuwa Sabrina Hamis,
ambaye kabla ya kesi kuanza kusikilizwa alikwenda hospitali kwa
matibabu ya mtoto huyo, ambaye hali yake ilibadilika ghafla akaamua
kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Kilumba, kulalamikia kesi
yake kufutwa kinyemela.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza lilianza kuwasaka watuhumiwa wote wawili akiwemo mshtakiwa na mwalimu aliyejifanya mlalamikaji.
Kaimu Kamanda, Kamishina Msaidizi wa Polisi Mwanza (ACP), Japhet Lusingu alisema
kuwa Aprili 13 mwaka huu watuhumiwa hao walikamatwa na kufikishwa
Mahakamani, baadaye akapata taarifa kwamba mwalimu huyo amefungwa miezi
sita kwa kuidanganya mahakama.
MTANZANIA
Watu 38 wameripotiwa kufariki jana
katika matukio mawili tofauti Mbeya na Shinyanga, ambapo tukio la Mbeya
limetokea Tukuyu, gari ndogo aina ya Toyota Hiace ilitumbukia mtoni na
baada ya kushindwa kukata kona wakati likiwa kwenye mwendokasi na tukio
ambalo RPC wa Mbeya, Ahmed Msangi alithibisha kutokea ambapo watu 19 walifariki.
Kamanda Msangi
amesema uchunguzi unaonesha gari hiyo ilipata ajali wakati ikikimbizwa
na madereva wa Coaster ambao waliiona ikipakia abiria kitu ambacho
madereva hao wa Coaster walikuwa wakipinga kwa kuwa walikuwa kwenye
mgomo kutokana na dereva mwenzao kupigwa faini ya 250,000/=
Katika tukio jingine Kamanda wa Polisi Shinyanga Justus Kamugisha
amethibisha kutokea tukio la watu 19 wanahofiwa kufariki kwa kufukiwa
na kifusi cha udongo katika machimbo madogo ya dhahabu kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha Mkoa huo.
Diwani wa Kata ya Lunguya ambako
limetokea tukio hilo amesema huenda idadi ya watu waliofukiwa ikawa
kubwa zaidi kutokana na eneo ambalo kifusi kimejifukia kuna watu wengi
waliokuwa wakiingia kuchimba dhahabu.
“Nimeshatuma
kikosi cha Polisi kwenda kusaidia kuokoa, lakini idadi ya watu
waliokufa tumeambiwa ni kuwa ni 19.. hatuna uhakika nayo..”—Kamanda Kamugisha.
MTANZANIA
Licha ya Rais Jacob Zuma kulaani vurugu zinazoendelea Afrika Kusini dhidi ya wageni vurugu hizo zimezidi kupamba moto na kuvuka mipaka ya nchi hiyo,
Raia wa Afrika Kusini wanaoishi
nakufanya biashara katika nchi za Msumbiji na Zimbabwe nao wameanza
kushambuliwa ambapo malori yenye namba za usajili za Afrika Kusini
yameshambuliwa Msumbiji, huku wanafunzi wa Vyuo vikuu Zimbabwe nao
wakiandamana na kufanya fujo kwa wafanyabiashara na wawekezaji waliopo
nchini humo.
Balozi wa Tanzania aliyeko Afrika Kusini amesema kuwa hakuna Mtanzania aliyeshambuliwa wala kuathirika na vurugu hizo.
Mmoja wa Watanzania ambao wanaishi
karibu na mpaka wa Afrika Kusini na Msumbiji amesema malori zaidi ya 100
yanayosafirisha makaa ya mawe yamekwama baada ya mpaka kufungwa.
MTANZANIA
Askofu Gwajima ameshitakiwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wenzake watatu kwa makosa
mawili ya kutoa lugha ya matusi na uzembe wa kuhifadhi silaha yake ya
moto ambayo anaimiliki kihalali.
Askofu huyo amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya matusi kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Kardinali Polycarp Pengo, lakini Askofu Gwajima alikana mashtaka yote mawili na kuachiwa kwa dhamana mpaka Mei 4 mwaka huu.
Kabla Askofu huyo hajafikishwa
Mahakamani nyumba yake ilizingirwa na Askari Polisi kwa muda wa saa nane
toka saa 12 asubuhi, milango ya nyumba hiyo ilikuwa imefungwa huku
waumini waliokusanyika nje ya nyumba hiyo pia wakiwashutumu Polisi kwa
kumng’ang’ania baba yao wa kiroho.
Ilipofika majira ya saa 6:03 walifika
baadhi ya viongozi wa Kanisa la Ufufuo na uzima pamoja na Mwanasheria wa
Askofu huyo na kufanya kikao kidogo na Askari Polisi hao ambapo baadae
waliondoka kuelekea Centre Police wakiwa na Askofu huyo, ambako
haikuchukua muda akatolewa na kupandishwa Mahakama ya Kisutu.
MWANANCHI
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Francis Isack amewasweka
ndani watendaji 16 wa vijiji na kata kwa madai ya kuzembea kusimamia
maabara za Sekondari ambapo mwenyewe amesema hiyo ni hatua ya
kukumbushana majukumu kwa kuwa wao ni Watendaji wa Serikali ambao
hawakupaswa kuzembea.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hatua hiyo ni ya kukumbushana majukumu yao waliyopewa na Serikali.
Amesema baada kuwahoji walitoa majibu mepesi kwamba wamezuiwa na madiwani kukusanya michango kwa wananchi.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda na wakati wowote hapa hapa www.tangakumekucha.blogspiot.com
No comments:
Post a Comment