MAHAKAMA
 ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru leo Katibu wa Jumuiya na 
Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa 
kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa 
upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.
********
Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.
Hati
 ya Mashitaka ya Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya Mashitaka matatu  lakini 
Julai 22 mwaka 2015, Hakimu Mkazi Mary Moyo  alitoa  uamuzi wa kumfutia 
shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda 
ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa 
uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu  katika mashitaka mawili 
yaliyosalia ambalo ni kosa la pili na la tatu .
Mahakama 
ya Hakimu Mkazi Morogoro  ilimfungia dhamana Sheikh Ponda baada ya 
kukubaliana na hati ya aliyekuwa  Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), wakati 
huo Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya 
Dar Es Salaam liloomba Mahakama hiyo imfungie dhamana mshitakiwa huyo 
chini ya Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai ya
 Mwaka 2002.
Hatua 
hiyo ya kufunguliwa kesi katika Mkoa wa Morogoro ilikuja ikiwa ni muda 
mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Agosti 19
 Mwaka 2013 saa Tatu asubuhi,  kumfutia kesi ya jinai  Na.144/2013 
katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano baada ya DPP kudai kuwa 
hana nia ya kuendelea kumshitaki katika kesi hiyo No.144/2013  kwa 
mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya
 mwaka 2002.
Hata 
hivyo baada ya hakimu Liwa kumwachilia huru,Ponda ambaye aliletwa 
mahakamani hapo saa 12 asubuhi na wanausalama wa polisi na magereza 
chini ya ulinzi mkali, alikamatwa tena na kupakizwa kwenye magari ya 
wanausalama hao ambapo baadhi ya wanausalama hao waliliambia gazeti hili
 kuwa wanampeleka Ponda mkoani Morogoro kwaajili ya kufunguliwa makosa 
matatu ya uchochezi, kufanya mkusanyiko haramu na kisha akarejeshwa 
gereza la Segerea Dar es Salaam , lakini baadae Uongozi wa Jeshi la 
Magereza uliamua kumuamisha Ponda kutoka Gereza la Segerea na 
kumuamishia Katika Gereza Moja Mkoani Morogoro.
Sheikh 
Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi,
 baada ya kuwasili kwa helikopta ya Jeshi la Polisi katika uwanja wa 
gofu mjini Morogoro.
Akisoma 
mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, 
Richard Kabate, Mwanasheria Kiongozi  wa Serikali, Bernard Kongola, 
alidai  kuwa Agosti 10, mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, 
Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa 
kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na 
BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
Alidai 
kuwa Sheikh Ponda ambaye anatetewa  na wakili wa kujitegemea Juma Nassor
 aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na 
kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge
 milango na madirisha wawapige.
Ilielezwa
 kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi 
Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa Mei 9, mwaka 2010, ambayo 
ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.
Katika 
shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo 
la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali 
ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi
 ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya 
wakazi hao ni Waislamu.
Kwamba, 
Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya hivyo kwa 
wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya 
uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa
 huko ni Wakristu.
Shitaka 
la tatu ambalo linafafana na lile la pili, ambalo nalo linadaiwa 
kutendwa Agosti 10, mwaka huu, ambapo kauli ya Ponda inadaiwa kuumiza 
imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni
 ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.
Oktoba 18
 mwaka 2012, Ponda na wenzie 49 walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu 
Mkazi Kisutu kwa Mara ya kwanza   wakikabiliwa na makosa matano, kosa la
 kwanza ni la kula njama, kujimilikisha mali, kuingia kwa jinai katika 
kiwanja cha Chang'ombe  Markas,wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. 
Milioni 59 na kosa la uchochezi ambapo katika kesi hiyo Jamhuri ilikuwa 
ikiwakilishwa na wakili Mwandamizi wa Serikali , Tumaini Kweka .Mahakama
 pia iliwafunga dhamana ya Ponda na mshitakiwa wa pili tangu 0ktoba 18 
Mwaka 2012 hadi siku Kesi hiyo iliyotolewa hukumu Mei 9 Mwaka 2013.
Mei 9 
mwaka 2013 Hakimu Mkazi Victoria  Nongwa akitoa hukumu yake katika kesi 
hiyo ya Ponda na wenzake alisema anawaachiria huru washitakiwa 49 
 kwasababu upande wa jamhuri  umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi yao na 
kwamba anamtia hatiani Ponda kwa kosa moja tu  la kuingia kwa jinai na 
kwamba na anamuachiria huru katika makosa manne yaliyosalia kwasababu 
pia jamhuri ilishindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya Ponda.
Sheikh 
Ponda alikataa rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga 
hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mei 9 mwaka 2013 ambapo alishinda 
rufaa yake.
Hata 
hivyo siku Chache baada ya Kufungwa Kifungo hicho cha nje Mei 9 mwaka 
2013, Ponda alikwenda Mkoani Morogoro na kufanya mkutano ambao alidai wa
 Kutenda makosa ya jinai ambao alikamtwa  Agosti Mwaka 2013 na kuwekwa 
chini ya ulinzi na kufunguliwa Kesi Mahakama ya Kisutu Na.144/2013 
ikafutwa na DPP na ndipo akafunguliwa kesi hiyo Mkoani Morogoro ambayo 
imetolewa hukumu Leo na kuachiwa huru.
CHANZO : OTHMANI MICHUZI