Saturday, November 21, 2015

MAMLAKA YA MAJI TANGA YALIA NA WEZI WA MIUNDOMBINU



Tangakumekuchablog
Tanga, MAMLAKA ya Maji Tanga (Tanga Uwasa) imedai kukabiliwa na changamoto ya wizi wa miundombinu na uchakavu wa mabomba pamoja na uharibifu wa chanzo cha maji.
Madai hayo yametolewa Leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Joshua Mgeyekwa wakati wa kikao cha Wadau kukusanya maoni kwa ajli ya mpango mkakati kwa mwaka 2015 -2020 na kusema kuwa hali hiyo inarejesha nyuma jitihada ya mamlaka kusambaza maji hadi vijijini.
Alisema wizi wa mifuniko ya mashimo ya maji taka na miundombinu ya ya maji imekuwa kikwazo cha kuyafikia malengo hivyo kuwataka wadau kushirikiana na tatizo hilo ili kuweza kuyafikia malengo mamlaka iliyojiwekea.
“Ndugu wadau tumekutana hapa sisi kueleza ya kwetu lakini nanyi tutaka kusikia maoni yenu kwetu---changamoto zinazotukabili nadhani hata nanyi zinawaathiri” alisema Mgeyekwa na kuongeza
“Kwa pamoja tushirikiane ili kuiwezesha mamlaka kuyafikia malengo yake ya kuwafikishia maji safi wananchi vijijini ambako kwa sasa ndio dira yetu” alisema
Alisema kutokana na mji kukua kwa kasi na mahitaji kuwa makubwa, mamlaka inangalia kuwa na chanzo chengine cha maji badala ya kutegemea kimoja ambacho kimekuwa kikihudumia maeneo mengi.
Alisema chanzo hicho cha Mabayani kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya uharifu mkubwa ikiwa na pamoja na ukataji miti na uchimbaji wa madini na kusababisha upungufu wa maji.
Alisema kumejitokeza wimbi la ukataji miti na uchmbaji wa madini karibu na  chanzo cha maji na kusababisha upungufu mkubwa wa maji nyakati za kiangazi hivyo kuwataka wadau kushirikiana na mamlaka ili kutokomeza wimbi hilo.
“Uchimbaji wa madini na ukataji wa miti karibu na chanzo cha maji limekuwa tatizo sugu----kwa muda mrefu tumekuwa tukisema na kuweka ulinzi masaa ishirini na nne lakini bila na nyinyi hatuwezi kufanikiwa” alisema Mgeyekwa
Mkazi wa Mikanjuni, Pitter Mohammed, ameitaka mamlaka hiyo kuongeza vituo vya huduma kwa wateja ili kupunguza msongamano na foleni kwenye ofisi ya ulipaji ndani ya mamlaka hiyo.
Alisema jiji zima liko na vituo viwili vya huduma kwa wateja jambo ambalo inakuwa kero wakati wa ulipaji wa Ankara mwisho wa mwezi na kusababisha foleni kubwa na kuwa kero.
Alisema ili kuweza kufanikisha malengo ya mamlaka ya maji iliyojiwekea, Mgeyekwa aliwataka wananchi na wadau wa maji kushirikiana na mamlaka hiyo katika kuendeleza utoaji wa huduma nzuri.
                                           Mwisho

Picha nambari DSCN1623jpg hadi picha nambari DSCN1627jpg, Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita akizungumza katika kongamano la wadau wa maji (Tanga Uwasa) lililofanyika juzi Tanga.

 Mkazi wa Mikanjuni kata ya Mabawa Tanga, Pitter Mohammed akizungumza katika kongamano la wadau wa mamlaka ya maji safi Tanga (Tanga Uwasa) lilifanyika leo.
M ganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita akizungumza katika kongamano la wadau wa maji (Tanga Uwasa) lililofanyika Leo Tanga.





No comments:

Post a Comment