Monday, November 16, 2015

WAOKOLEWA BAADA YA KUISHI KWA SIKU 41 CHINI YA ARDHI

Mmoja wa wahanga hao akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama. 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu 5 kati ya 6 waliyokuwa wamefunikwa na kifusi kwa siku 41 katika machimbo madogo wa nyangalata wilayani kahama mkoani shinyanga wameokolewa wakiwa hai. 
Wakizungumza leo na kahama fm wakati wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mji wa kahama, wahanga hao wamesema hali hiyo imewakuta katika harakati za kuwaokoa wenzao waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika machimbo hayo. 
Wahanga hao ni Onyiwa Kanyimbo(55),Msafiri Jerald(38) Amosi Muhangwa(25), Chacha wambura(53) na Joseph Burule(44) na aliyefariki dunia ni Mussa Supana. 
Wamesema walikuwa wakiishi kwa kunywa maji, na kula magome ya miti pamoja na mende hali iliyowasababisha kuendelea kuwa hai kwa siku 41 hadi jana jioni walipookolewa. 
Menaja wa mgodi mdogo huo Amosi Mbanga amesema timu ya mafundi ilifanya utafiti na kugundua kuna sauti za watu zikiita na kuamua kupeleka uwokawaji kushirikiana na serikali pamoja kampuni acaica na kufanya uokowaji huo ulichukua masaa 24. 
Naye kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya kahama Dk. Jibai Mkama amethibitisha kuwapokea wahanga hao na kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri wakiwa bado wanapatiwa matibabu katika hosspitali hiyo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment