Kenya nako wameamua, ni marufuku bodaboda katikati ya Jiji Nairobi..
Katikati ya Jiji la Dar es Salaam hili
zoezi lilianza muda mrefu zaidi ya mwaka sasahivi, ambapo ilipigwa
marufuku kabisa madereva wa bodaboda na Bajaji kuonekana wakisafirisha
wateja wao kuingia katikati ya Jiji, headlines leo zinaigusa Nairobi
Kenya !! Bodaboda marufuku katikati ya Jiji.
Hiyo stori imeripotiwa na Kituo cha TV cha K24 ambapo
madereva wa bodaboda wenyewe wameonekana kulalamikia agizo hilo
wakisema kwamba wanazuiwa kuingia katikati ya Jiji lakini hawajaoneshwa
wapi ni eneo rasmi haswa ambapo wanatakiwa kufanya shughuli zao.
Kingine ambacho kimetengazwa Nairobi ni
kwamba mkikamatwa mnakatisha katikati ya Nairobi, abiria pamoja na
dereva wote mnapigwa faini…
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment