Tuesday, November 24, 2015

SEKTA YA WAZIWA NA CHANGAMOTO ZAKE


Tangakumekuchablog

Tanga,IMEELEZWA kuwa sekta ya Maziwa nchini  inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya elimu ya ufugaji na miundombinu ya ufikishaji maziwa viwandani.

Akizungumza katika kongamano la Kimataifa la wafugaji wa ngombe wa maziwa na wafanyakazi lililofanyika leo Tanga, Mratibu wa Miradi kutoka kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh, Chales Tumaini, alisema wafugaji wengi wako na changamoto katika ufugaji wao.

Alisema wafugaji wengi hawana elimu ya ufugaji wa ngombe wa maziwa na badala yake wamekuwa wakiendesha kwa mazoea jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma kwenye sekta ufugaji ng'ombe wa maziwa.

“Sekta ya ufugaji wa ngombe wa maziwa unakuwa kwa kasi barani Afrika---lakini kuna changamoto kubwa kwa wafugaji hasa wadogo wadogo ambao hawana elimu ya kutosha ya ufugaji” alisema Tumaini na kuongeza

“ Usafi pia ni moja ufugaji mahiri na wengi wamekuwa wakitumia vyombo ambavyo sio rasmi na maziwa yakifika kiwandani na kupimwa yanapungua ubora na mfugaji kupata hasara” alisema

Kwa upande wake Mkufunzi na Mshauri wa wafugaji wa maziwa kutoka Uholanzi, Ciska Anema, aliwataka wataalamu wa mifugo kuwafuata wafugaji mashambani.

Alisema wafugaji wengi wa mashamabani hawana elimu ya ufugaji wa ngombe wa maziwa na badala yake wamekuwa wakifuga kienyeji na kutopata faida na hivyo kuiona sekta hiyo haina tija.

Aliwataka wataalamu na wafanyakazi viwandani kuwatembelea wafugaji wao na kuwaelimisha ufugaji mahiri ambao utaweza kuwaongezea kipato na kuacha kusubiri maziwa viwandani.

“Wamiliki wa viwanda wanapaswa kuwatembea wafugaji wao mashambani na kuwapa elimu nzima ya ufugaji ----hii itawaongezea wingi wa upatikanaji wa maziwa na faida” alisema Anema

Alisema wafugaji wengi wako na shauku ya kuendesha mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa lakini wanashindwa kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya ufugaji.

                                                  Mwisho


, Mkufunzi na Mshauri wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka Uholanzi, Ciska Enema, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la wafugaji na wafanyakazi wa sekta ya maziwa lililofanyika Tanga leo

No comments:

Post a Comment