Friday, November 27, 2015

TRA KUMEKUCHA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa  wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.
Maafisa hao, ambao majina yao yamehifadhiwa  ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.
Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
 Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa 
akiagana na viongozi wa TRA na TPA.

No comments:

Post a Comment