Monday, November 16, 2015

KUTOKA MUHIMBILI, DAR ES SALAAM

Kingine kilichonifikia kutoka hospitali ya Muhimbili ni hiki….

Zikiwa ni siku chache baada ya mashine za MRI kuanza kufanya kazi katika hospitali ya Taifa Muhimbili, taarifa iliyonifikia leo kutoka kwa uongozi wa hospitali hiyo huduma hizo zimesimamishwa kwa muda kuanzia leo kwa ajili ya matengenezo.
Mashine hizo zilianza kufanya kazi baada ya agizo la Raid Dk.Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kukuta mashine zote mbili za MRI na CT Scan zikiwa mbovu
Wiki iliyopita huduma za MRI zilianza kufanya kazi baada ya mashine hiyo kutengenezwa lakini siku chache zilizopita ilionekana kuwa na hitilafu ya kiufundi ambayo inahitaji matengenezo.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaesha amesema tayari uongozi wa hospitali unawasiliana na kampeni iliyopewa kazi ya kutengeneza ili kurekebisha hitilafu hizo.
Barua yao ilisomeka hivi..
MUHIMBILI
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment