Monday, November 16, 2015

MAFURIKO TANGA



Wakazi wa Magaoni kata ya Mabawa Tanga wakiangalia nyumba zao zilizozingizwa na maji kufuatia  mvua  kubwa iliyonyesha usiku wa leo na  kusababisha kuyahama majumba yao.
Mvua hiyo inayodaiwa kunyesha kuanzia saa 9 usiku inasemekana kuw akubwa kuwahi kunyesha kwa siku za hivi karibuni.
Baadhi ya wanaharakati na kada mbalimbali wamewataka wananchi wanaoishi mabondeni na kando kando ya mabwawa kuchukua tahadhari na kuchimba mifereji ili kuyawezesha maji kupita kwa urahisi bila kuathiri majumba yao.
Kwa upande wa Serikali imekuwa ikitoa tahadhari kwa watu kuacha kujijengea nyumba bila kufuata taratibu za mipangomiji jambo ambalo limekuwa likipelekea kujenga kienyeji na nyakati za mvua maji kuingia majumbani mwao






1 comment: