Thursday, November 26, 2015

TANESCO TANGA YATOA UFAFANUZI KERO YA UMEME



Tangakumekuchablog
Tanga, KUFUATIA kukatika na kuwaka umeme mara kwa mara jijiji Tanga, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa ufafanuzi na kusema kuwa hiyo ni kutoka na uhaba wa waji kutoka katika vyanzo vyake vya Kidato na Mtera.
Afisa Uhusiano Huduma kwa Wateja Tanesco Tanga, Monica Mabada, ameiambia Tangakumekuchablo kuwa uhaba wa maji katika chanzo cha Mtera na Kidato Shirika hilo linalazimika kufanya jitihada mbadala ili huduma ya upatikanaji umeme uendelee.
Alisema kwa sasa Shirika la Umeme Tanzania liko katika mchakato wa kuhakikisha kero kwa wateja wa majumbani na viwandani inaondoka kwa kutafuta vyanzo vyengine hadi mabwawa hayo yatakapojaa maji.
“Kukatika umeme mara kwa mara kama unavyosema huwa mara nyingi mafunzi  wako kazini si usiku wala mchana----hitilafu za umeme mara nyingi hutokea usiku” alisema Mabada na kuongeza
“Ukatikaji wa umeme ni mafundi wako kazini na hakuna tatizo lolote zaidi ya kusema vyanzo vyuetu vimepungukiwa na maji lakini sio kuwa ni tatizo la wateja kupatwa na kitisho” alisema
Akizungumzia miundombinu ya umeme, Afisa huyo alisema kuna marekebisho ya vifaa katika Transfoma yake kubwa ya Majanimapana na hivyo wako katika mchakato wa mwisho wa kukamilisha.
Alisema kumalizika kwa kubadilishwa kwa kifaa hicho wakazi wa jiji la Tanga watakuwa na uhakika wa umeme maradufu na hivyo kuwataka kuwa wavumilivu kipindi hiki cha mchakato wa marekebisho ya miundombinu yake.
                                                  Mwisho

No comments:

Post a Comment