Friday, November 13, 2015

BIMA YA AFYA (NHIF) YATOA MASHUKA KWA HOSPITALI YA BOMBO



Tangakumekuchablog
Tanga, MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza ameyataka mashirika na taasisi za watu binafsi kuisaidia hospitali ya Bombo ili kuweza kukabiliana na changamoto inazo ikabili.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mashuka kwa ajili ya hospitali ya Bombo na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mahiza amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi hivyo kutaka kusaidiwa.
Amesema wagonjwa wengi wamekuwa wakikimbilia hospitali hiyo Ilhali hospitali za Wilaya zipo hivyo kuwa chanzo cha kukabiliwa na wimbi la wagonjwa na msongomano wa watu wengi.
Kwa upande wake Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga, Ali Mwakababu, amesema msaada huo umekuja baada ya kuona changamoto za wagonjwa waliolazwa  katika hospitali hiyo.
Amesema msaada huo ni muendelezo wa Bima ya Afya kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Elimu, Afya na Mazingira.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa angakumekuchablog

No comments:

Post a Comment