Wednesday, November 25, 2015

MTOTO ALIYEKAMATWA NA SAA IKIDHANIWA BOMU, ISHU IMERUDI TENA MAHAKAMANI

Mtoto aliyekamatwa na saa wakidhani bomu, ishu imerudi tena meza ya Mahakama Marekani !!

Hii stori ilipewa uzito wa aina yake, kulikuwa na upande mzuri na upande mwingine haukuwa mzuri… najua kama uliifatilia kwa ukaribu utagundua kwamba kulikuwa na headlines zikihusishwa na kukamatwa kwake na ishu ya udini..
Lakini kwenye upande mzuri ilikuwa dunia kuutambua na kuuheshimu ubunifu wake, akapokea pongezi nyingi ikiwemo kutoka kwa Rais Obama na Mark Zuckerberg… sio kila mtu anaweza kubuni saa kama aliyobuni Ahmed Mohamed, kijana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Texas Marekani.
Ahmed Mohamed akiwa na Rais Obama
Ahmed Mohamed alipokutana na Rais Obama
Familia haijaridhika, wamerudi Mahakamani na kudai fidia ya dola Milioni 15 kutokana na kitendo cha mtoto wao kukamatwa kimakosa akihisiwa kuwa na bomu wakati ilikuwa ni saa ambayo aliibuni mwenyewe na akaenda nayo shule… kingine ambacho familia inalalamika ni ishu ya Ahmed kukamatwa na kuhojiwa na Polisi bila wazazi wake kutaarifiwa.
Ahmed-Mohamed-Clock
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment