Friday, November 27, 2015

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Bingwa wa sura mbaya kapingwa Zimbabwe.. cheki maneno ya wanaompinga sasa !!

Hii stori imebeba uzito wake mkubwa tu, hicho kitu kilifanya vyombo vya habari vikubwa duniani kama CCTV, BBC na CNN kuripoti kuhusu stori ya shindano la watu wenye sura mbaya Zimbabwe !!
Mshindi alipatikana ambaye ni Mison Sere na alijikusanyia dola 500 zake, lakini unaambiwa watu walioingia kwenye shindano na kuukosa ushindi wana maneno yao kwamba Mison hastahili ushindi hata kidogo.
Mimi nina sura mbaya ya asili kabisa, Maison hana hiyo… yeye anaonekana na sura mbaya kama akifungua mdomo“- huyo ni mmoja wa washiriki waliokosa ushindi, anaitwa Masvinu.
ZIB BOYS
Huyu mwingine nae hataki kuamini kwamba kaukosa ushindi >> “Kwa hiyo ni lazima tusiwe na meno mdomoni ili tuwe washindi? Huu ni udanganyifu mkubwa“- Patrick Mupereki.
Japo hayo yote yameongelewa, Mison mwenyewe ana haya kuhusu mipango inayofatia baada ya ushindi wake >> “Tayari nimeanza kufanya show kwenye shule mbalimbali kuonesha ubaya wa sura yangu, natafuta nafasi nyingine zaidi ya kuonekana kwenye TV


Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment