Sunday, November 22, 2015

HOMA YA USAJILI UINGEREZA YAPANDA

Homa ya usajili haya, ndio majina ya wachezaji 10 huenda wakatua Arsenal na Mkenya ndani

Ikiwa homa ya dirisha dogo la usajili inazidi kuchukua headlines Tanzania, vilabu vikiendelea kusaka saini za wachezaji zinaowataka waongeze nguvu vikisoni mwao kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa December 15, nchini Uingereza homa ya dirisha dogo la usajili inazidi kuchukua headlines katika vilabu kadhaa ikiwemo Arsenal.
West-Brom-vs-Arsenal
Coquelin akitolewa nje baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya West Brom
Kwa kiasi kikubwa klabu ya Arsenal inahusishwa kufanya usajili wa mchezaji au wachezaji wanafasi ya kiungo, Arsenal kwa sasa ambayo inasumbuliwa na wachezaji wake kuwa majeruhi, hivyo inahusishwa kwa karibu kutaka kusajili wachezaji wa nafasi ya kiungo ambao ndio wengi wao majeruhi kikosi mwao.
Southampton-vs-Bournemouth
Victor Wanyama mwenye mpira
Kwa sasa Arsenal ina wachezaji watano ambao ni majeruhi Aaron Ramsey, Francis Coquelin, Mikel Arteta, Jack Wilshere na Alex Oxlade-Chamberlain ila inahusishwa kutaka kuwasajili Luiz GustavoChristoph KramerLucas BigliaWilliam CarvalhoGrzegorz KrychowiakCheikhou KouyateJames McCarthyEver Banega na mkenya Victor Wanyama anayekipiga katika klabu ya Southampton ya Uingereza miongoni mwa majina hayo usishangae kama jina moja wapo likijiunga na Arsenal mwezi January.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment