Tuesday, November 10, 2015

WACHEZAJI WA MAN UNITED WAMPACHIKA JINA LA UTANI KOCHA WAO

Utamaduni wa wanafunzi kuwatunga majina waalimu wao ulikuwepo toka zamani na mara nyingi mwalimu anaweza kutungwa jina ambalo yeye halijui ila kutokana na tabia na muonekano wake basi wanafunzi hupenda kumtunga jina linaloendana na tabia zake kama ni mkali usishangae ukisikia akipewa jina la ajabu kama mnoko na kadhalika.
PAY-Man-United-arrive-at-The-Lowry-Hotel
Stori zilizotoka mtandaoni ni kuwa wachezaji wa klabu ya Manchester United wameamua kumtunga jina kocha wao raia wa Uholanzi Louis van Gaal, wachezaji wa Man United wamempa jina kocha wao la “Daisy” kutokana na tabia yake ya kuendesha gari taratibu akiwa anawasili katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo Carrington na kukwepa vishimo vidogo vidogo.
_82305410_man_united_reuters
Jina hilo la ‘Daisy’ linatoka katika movie iliyowahi kutamba miaka ya nyuma ya ‘Driving Miss Daisy’ wachezaji hao wamempa jina la utani kocha huyo ambaye pia wanamtaja kama muoga na anaendesha gari taratibu sana na mwendo wa gari yake ukifananishwa na mwendo wa Konokono. Hata hivyo Louis van Gaal ni kocha ambaye anafahamika kwa tabia yake ya ukali na misimamo.
Driving-Miss-Daisy-1989--Front-Cover-75825
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment