Sunday, November 29, 2015

KIPINDUPINDU KITAONDOKA HALI KAMA HII TANGA?

 Takataka zikiwa zimerundikana na kuzagaa hadi kuziba njia barabara ya 16 Soko la Mlango wa Chuma Masiwani Tanga na kusababisha kero kwa wakazi wa eneo hilo na kutoa harufu kali kipindi hiki cha kuzuka ugonjwa wa kipindupindu .
Inadaiwa kuwa mawakala wa zabuni wanaoshughulikia usafi hususani katika masoko wamekuwa wakilaumiwa kwa kuacha takataka hadi kurundikana na kufikia kiwango cha kuziba barabara .
Hii imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika masoko na kufanya madampo hali ambayo inatishia kuzuka kwa magonjwa ya Kipindupindu na mengineyo. 
Wanaharakati Tanga wameiambia Tangakumekuchablog kuwa kuna uzembe na kutofuatilia na hivyo kushauri hatua madhubuti kutekelezwa.





No comments:

Post a Comment