MHUBIRI MAARUFU DUNIANI TB JOSHUA WA NIGERIA ATUA DAR ES SALAAM KUSHUHUDIA DKT MAGUFULI AKIAPISHWA
Mhubiri maarufu TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua 
jijini Dar es salaam leo  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa 
Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara
 tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB 
Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho 
 Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa 
uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB 
Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kumpata Magufuli kama mrithi 
wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na 
Fanaka tele katika awamu hii mpya.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki 
 TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu 
jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam 
 tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John 
Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
 Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na TB Joshua wa kanisa la Church 
of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
Picha na Freddy Maro


No comments:
Post a Comment