HADITHI hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Kampuni ya mabasi ya abiria FREYS LUXURY COACH, ifanyayo safari zake kati ya Tanga hadi Sindida kila siku kupitia Moshi, Arusha na Babati, na hufanya hivyo kila siku kutokea Singida kwenda Tanga kupitia Babati, Arusha, Moshi hadi Tanga, kwa mawasiliano, 0622 292990
MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA
UKINGONI 13
ILIPOISHIA
Polisi hao wakaanza kupima
ajaIi hiyo na kuzuia magari mengine yapite kando. Baada ya kupima ajali polisi
mmoja alimwambia dereva wa gari jingine atoe kadi ya gari lake.
“Iko nyumbani” aliwambia.
“Kwanini hutembei nayo?”
“Niliisahau”
“Leseni yako iko wapi?”
Jamaa alijipapapasa kisha
akasema.
“Leseni pia nimeisahau
nyumbani”
SASA ENDELEA
“Kila kitu Umesahahu
nyumbani? Yaani unaendesha gari bila kuwa na leseni?”
“Sio kama sina, nimeisahau
tu”
“Tutaaminije kama unayo
leseni au huna?”
“Nitakwenda kuichukua”.
Kombo alikuwa yuko ofisini
kwake akisubiri ruhusa ya kurudi tena nyumbani kwa Waziri Mkuu kumhoji kuhusu
utata uliojitokeza kati ya maelezo yake na maelezo ya Mzee Amrani, simu yake
ikaita juu ya meza.
Aliunyakua mkono wa simu na
kuuweka sikioni kwake, akasema.
“Hello!”
“Kuna gari limekamatwa na
polisi wa usalama barabarani limefanana na lile lililoshukiwa, ni aina ya Land
Cruiser la rangi nyeupe. Nimewaambia walilete hapa” Kombo aliitambua sauti hiyo
kuwa ilikuwa ya afisa upelelezi.
“Limekamatwa wapi?” Kombo
akauliza.
“Limekamatwa Kimara,
liligongana na gari jingine lakini limegundulika kuwa ni la waziri mkuu”
“Ni nani aliyekuwa
akiliendesha?”
“Ni dereva wake”
“Ningependa nimuone”
“Hilo gari litaletwa sasa hivi pamoja na huyo
dereva”
Waziri Mkuu alikuwa
amesharudi nymban kwake alipopigiwa simu na dereva wake Kidasi Athumani.
“Mzee nimepata ajali, gari
limekamatwa na polisi” Kidasi alimwamba Wazri mkuu kwenye smu.
“Umegonga au umegongwa?”
“Nimegonga gari kwa nyuma.
Gari lilifeli breki”
“Kuna aliyejeruhiwa?”
“Hakuna aliyejeruhwa”
“Ajali imetokea wapi?”
“Kmara. Nilikuwa narudi
kutoka Kibaha”
“Ilikuwa ajali kubwa?”
“Si kubwa lakini gari nililoligonga
limebonyea kwa nyuma”
“Polisi wamekwambia nini?”
“Wamenikamata”
“Umewambia kuwa gari hilo ni langu?”
“Nmewambia”
“Sawa. Waache wafuate
taratibu zao halafu utanifahamsha”
“Sawa mzee”
Waziri Mkuu aliiweka simu
yake juu ya meza kisha akamtazama mke wake.
“Kidasi amepata ajali”
akamwambia.
“Wapi?”
“Kimara”
“Amegonga au amegongwa?”
“Amegonga”
Mke wa Wazir Mkuu akaguna.
“Wiki hii ni ya mkosi kwetu,
sijui ni kitu gani kinataka kututokea”
“Yuko kituo cha polisi,
nimemwamba anifahamishe kitakachoendelea. Kama mwenye gari atataka kulipwa
tutamlipa, kama atataka tuendelee na kesi
sawa”
“Vizuri ni kumlipa tu”
“Akitaka tumlipe gharama za
matengenezo tutamlipa”
“Kabla ya Kidasi kukupigia
simu ulikwa unataka kunieleza kitu”
“Nimearifiwa kuwa wale
wapelelezi wanataka kurudi tena kutuhoji kuhusu kuuawa kwa Pili”
“Waje tena mara ya pili?“
“Ndio, na mimi nimeshangaa”
“Labda wamegndua kitu”
“Kitu gani?”
“Kitu chochote tu. Unadhani
wanakuja bure”
“Nmewambia na waje tu”
“Watakuja saa ngapi?”
“Nimewambia baada ya masaa
mawili nitakuwa nyumbani. Wanaweza kuja wakati wowote kutoka sasa”
*************
Kidasi alishangaa alipoona
akipelekwa katika ofisi ya idara ya upelelezi makao ya polsi. Aliingizwa katika
ofisi Thabit Kombo na kuanza kukabiliana na maswali ambayo hayakuhusiana na ajali
iliyotokea.
“Wewe upo katika ajira ya
serikali au binafsi?” Kombo alimuuliza.
“Niko katka ajira binafsi.
Waziri Mkuu aliniajiri niwe dereva wa gari zake”
“Gari zake binafsi sio?”
“Ndio”
“Unamuendesha nani?”
“Zile gari ni kwa ajili ya
shughuli za shamba lake lililoko Kibaba”
“Sawa. Ni wakati gani
unaingia kazini, na wakati gani unatoka kazini?”
“Sina muda maalum wa kuingia
au kutoka kazini. Kuna siku naingia kazini saa kumi na moja alfajir kwa ajili
ya kwenda Kibaha kufuata maziwa ya ngombe. Ninakuwa kwenye gari nyengine. Siku
nyngine naingia kazini saa mbili asubuhi”
“Na kutoka?”
“Pia sina muda maalum,
inategemea nitakapomaliza kazi ninazotumwa”
“Unaweza kuwa na gari hilo hadi saa ngapi?”
“Wakati mwingine hadi saa nne
usiku”
“Hebu niambie jana ulitoka
saa ngapi kazini?”
“Nilitoka saa nne usiku”
“Ulikuwa umekwenda wapi?”
“Kibaha”
“Na uliondoka hapa jijini saa
ngapi?”
“Niliondoka saa kumi”
“Hilo gari liko wapi?”
“Limeletwa hapa makao ya
polisi”
“Hebu twende nikalione”
Kombo na Kidasi walitoka
ofisini wakaenda lilikokuwa gari hilo.
Kombo alilikagua. Alifungua
mlango wa nyuma na kulitazama ndani kisha akafunga mlango.
“Kwa hiyo jana ulikuwa na
gari hili hadi saa nne usiko?”
“Hili gari nilikuwa nalo
kuanzia asubuhi hadi saa kumi ambapo nilichukua gari jingine ambalo tunabebea
ndoo za maziwa”
“Sio hili?”
“Hapana. Kuanzia saa kumi
hadi saa nne usiku nilikuwa na gari jingine, sio hili”
itaendelea kesho usipitwe na uhondo huu hapahapa tangakumekucha
No comments:
Post a Comment