HADITHI
MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA
UKINGONI 3
ILIPOISHIA
Hospitali yenyewe ilikuwa
Masaki. Ilikuwa hospitali kubwa ya binafsi iliyokuwa ikiendeshwa na mzalendo wa
Kitanzania. Ilikuwa ikitumiwa zaidi na mawaziri na waheshimiwa wengine ndani ya
serikali.
Baada ya uchunguzi uliochukua
dakika kadhaa kutoka katika sampuli ya damu ya binti wa Waziri Mkuu,
iligunduliwa kuwa binti huyo hakuwa akisumbuliwa na malaria.
Madakatari walichukua vipimo
vingine ambavyo navyo vilionesha kuwa Sofia
hakuwa na tatizo lolote la kiafya.
Matokeo hayo licha ya
kuutuliza moyo wa Sofia, yalimshangaza mama yake. Sofia alipoulizwa anajisikiaje alijibu kuwa
alikuwa anajisikia vizuri.
“Alisema kichwa kilikuwa
kinamuuma sana”
Mama yake akawambia madaktari.
“Lakini sasa hivi hakiumi
tena” Sofia
akadakia.
“Anaonekana kuwa na afya
njema. Uchovu pia unaweza kusababisha kuumwa kichwa. Hili si tatizo kubwa hasa
kama linatokea kwa mara moja” Daktari alimwambia mama yake Sofia.
SASA ENDELEA
Sofia hakupata matibabu
yoyote akarudishwa nyumbani. Dereva alipewa shilingi elfu hamsini na waziri kwa
ajili ya usafiri wake kabla ya kuondoka.
“Ninashanga kusikia kuwa Sofia hana malaria” Waziri
alimwambia mke wake akiwa chumbani.
“Hata mimi nimeshangaa na
mwenyewe anasema anajisikia vizuri”
“Sasa amepatwa na tatizo
gani?”
‘Inabidi tuendelee kumfanyia
uchunguzi zaidi”
“Okey, sasa hili suala
jingine tutalitatua vipi?”
“Sijui wewe mwenzangu umewaza
nini?”
“Kusema kweli kichwa changu
kimevurugika sana.
Ni afadhali ingegundulika kuwa Sofia
ana malaria”
“Itaonekana kwamba aliua kwa
kukusudia”
“Lakini ni lazima kutakuwa na
tatizo, Sofia
hawezi kumtoboa mtu na kumfyonza damu hadi kumuua”
“Na inaonekana alifanya hivyo
bila kujielewa”
“Kwa hiyo ni lazima kuna
tatizo”
**************
“Ninashangaa kusikia kuwa
Sofia hana malaria” Waziri alimwambia mke wake wakiwa chumbani.
“Hata mimi nimeshangaa na
mwenyewe anasema anajisikia vizuri”
“Sasa amepatwa na tatizo
gani?”
‘Inabidi tuendelee kumfanyia
uchunguzi zaidi”
“Okey, sasa hili suala
jingine tutalitatua vipi?”
“Sijui wewe mwenzangu umewaza
nini?”
“Kusema kweli kichwa changu
kimevurugika sana.
Ni afadhali ingegundulika kuwa Sofia
ana malaria”
“Itaonekana kwamba aliua kwa
kukusudia”
“Lakini ni lazima kutakuwa na
tatizo, Sofia
hawezi kumtoboa mtu na kumfyonza damu hadi kumuua”
“Na inaonekana alifanya hivyo
bila kujielewa”
“Kwa hiyo ni lazima kuna
tatizo”
“Sasa tatizo limezaa tatizo
na tunatakiwa tulishughulikie usiku huu huu”
“Sikiliza mke wangu, siwezi
kumtia binti yangu kwenye matatizo ya kiserikali, si unajua tuhuma za mauaji ni
kubwa. Na pia siwezi kujitia mimi mwenyewe katika matatizo ya kiserikali, bado
ninahitaji niwe waziri mkuu kama nilivyo,
nisingependa nipate kashfa yoyote”
“Umekusudia kufanya nini”
“Hili tatizo limetokea kwa
bahati mbaya na linaweza likatuweka mahali pabaya sisi sote. Kwa hiyo nimeona
nifanye kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Si kitu kizuri lakini ni
lazima nikifanye haraka iwezekanavyo ili kuokoa jahazi”
“Ningependa kukisikia ili
tushauriane”
“Nataka niuchukue huu mwili
wa Pili nikautupe sehemu nyingine usiku huu”
“Ukishautupa itakuwaje?’
”Ninataka ionekane kuwa Pili
hakuuawa nyumbani kwangu”
“Ni wazo zuri…”
“Mwili wake utakapoonekana
asubuhi nitaeleza kuwa Pili aliondoka nyumbani kwangu saa moja usiku.
Alituambia kuwa anaumwa na kichwa na alitumia usafiri wake mwenyewe”
“Ni sawa. Katika kujinusuru
mpango huo unafaa”
“Sidhani kama kuna mtu
atatushutumu”
“Si rahisi”
“Polisi watachunguza na
wataona ameuawa na watu wengine”
“Mimi nakubaliana na wazo hilo”
“Sasa kama tumekubaliana acha
nibadili nguo, niubebe ule mwili niutie kwenye gari langu. Nitaendesha
mwenyewe. Ile gari yangu binafsi haijulikani sana, hakuna atakayeweza kunitambua”
“Halafu utakwenda kumtupa
wapi?”
“Nitatafuta sehemu yenye kiza
mitaa ya uswahilini. Hakuna atakayeniona usiku huu’
“Kwani hivi sasa ni saa
ngapi?”
Waziri aliitazama saa yake ya
mkononi.
“Sasa ni saa tano, inakaribia
kuwa na robo”
“Bado ni mapema mno,
ungesubiri angalau ifike saa saba. Kutakuwa kimya sana”
“Kusubiri hadi saa saba ni
kupoteza muda, huu mwili tunatakiwa tuuondoe haraka humu ndani. Sidhani kama
nitakosa sehemu nzuri muda huu”
“Sawa, basi wahi”
Waziri akabadili nguo. Alivaa
jinzi na tisheti. Kichwani alivaa pama ili kuficha uso wake.
“Umebadilika sana” mke wake alimwambia
na kuongeza.
“Si rahisi mtu kukutambua”
“Na kwa vile nitatumia gari
langu binafsi ndio sitatambulika kabisa”
“Sasa twende tukasaidiane
kumbeba”
Wakatoka chumbani. Walikwenda
stoo wakauchukua mwili wa msichana huyo na kutoka nao. Waliupakia kwenye gari
la waziri katika siti ya nyuma.
Waziri akafungua mlango wa
dereva akajipakia na kuliwasha gari.
“Ngoja niende” alimwambia mke
wake na kulitoa gari.
Kwa saa kadhaa Waziri Mkuu
alikuwa akizunguka na gari lake
katika
mitaa ya eneo la Kinondoni ambako Pili, msichana aliyeuawa na mwanawe alikuwa
anaishi.
Waziri Mkuu hakuwa akijua
Pili alikuwa akiishi katika mtaa gani lakini hilo halikuwa tatizo kwake. Mradi alikuwa
akijua kuwa alikuwa akiishi katika eneo hilo
alitaka kuuacha mwili wake mahali popote tu ili iwe rahisi kutambuliwa na ndugu
na jamaa zake.
Ingawa ulikuwa usiku mwingi
baadhi ya mitaa ya eneo hilo
ilikuwa bado ina harakati za watu. Baadhi ya mitaa mengine iliyokuwa iko kimya
ilikuwa imeng’arishwa na taa za barabarani pamoja na taa za majumbani, hali
iliyosababisha waziri ashindwe kuutelekeza mwili huo aliokuwa ameupakia kwnye
gari.
Katika kuzunguka zunguka
kutafuta sehemu tulivu iliyo kimya na yenye kiza alitokea katika eneo la shule
moja ya msingi ambayo ilikuwa na kiwanja cha mpira.
Kiwanja hicho kilikuwa kama jangwa lililoachwa pekee. Karibu na kiwanja hicho
kulikuwa na majengo ya shule yaliyokuwa kiza na kimya.
Waziri akaona mahali hapo
palikuwa muafaka kuuacha mwili wa Pili kwani hapakuwa na nyumba za watu karibu
na palikuwa kiza. Aliliingiza gari ndani ya eneo la kiwanja hicho akavipita
kidogo vyuma vya magoli ya upande mmoja kisha
akalisimamaisha gari.
Alibaki kwenye siti kwa
dakika kadhaa kuangalia kama kutatokea mtu
yeyote. Alipoona hakukuwa na mtu yeyote aliyejitokeza akafungua mlango wa gari
na kushuka.
Alikwenda kwenye mlango wa
siti ya nyuma akaufungua. Aliuvuta mwili wa Pili akautoa kwenye gari. Akiwa
ameushikilia mikononi alikwenda pembeni mwa goli, mahala ambapo palikuwa na mti
wa mwembe.
Alitaka auweke mwili huo
chini ya mwembe uliokuwa hapo lakini ghafla akashitushwa na mwanga wa tochi
uliokuwa ukimmulika. Mwanga huo ulitokea sambamba na mlio wa mabuti uliosikika
kutoka nyuma yake.
Ule mshituko uliufanya mwili
wake usisimke. Akiwa bado ameushikilia mwili wa Pili aligeuka haraka na
kutazama nyuma.
“Wewe nani na unafanya nini
mahali hapo?” Sauti nzito ya mtu aliyekuwa akija kwa haraka nyuma yake
ilimtatanisha.
Akagundua mara moja kuwa
alikuwa mlinzi wa ile shule. Alikuwa amevaa kama
askari wa makampuni ya ulinzi akiwa na kofia na mabuti.
Mkono mmoja alikuwa ameshika tochi iliyokuwa
ikimmulika na mkono mwingine alishika sime ambayo tayari alikuwa ameipunga juu.
Alikuwa kama hatua kumi na
tano hivi nyuma ya waziri.
Ule mwanga wa tochi sasa
ulikuwa ukimpiga
waziri usoni.
Kile kitendo cha kufumwa
akiwa katika hatua ya kuutupa mwili huo kilimfanya ababaike na kutaharuki.
Kadhalika ule mwanga wa tochi uliokuwa ukimmulika usoni ulimchanganya
zaidi.
“Nimekuuliza wewe ni nani na
unataka kufanya nini katika eneo hili?’ Mlinzi huyo alimuuliza tena waziri huku
akikaza mwendo kumfuata.
Alikuwa amemkaribia sana.
Itaendelea kesho hapahapa tangakumekuchablog.
KUMEKUCHA UPYA
No comments:
Post a Comment