Saturday, September 17, 2016

AMINI USIAMINI, HUU NDIO UKWELI

Mamba mkubwa Big Daddy kufanyishwa ndoa Mombasa

Big Daddy
Mamba VillageMmoja ya mamba wakubwa zaidi duniani kwa jina Big Daddy, ambaye anafugwa katika katika Mamba Village, mjini Mombasa, atafungishwa ndoa rasmi na wake zake wawili, Salma na Sasha.
Hafla hiyo ya kipekee inatarajiwa kufanyika Aprili tarehe 29 mwakani mjini Mombasa.
Mamba huyo ana uzani wa tani moja na anaaminika kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100.
Waandalizi wa ndoa hiyo wanasema wameamua kumsaidia Big Daddy afanye harusi baada ya kuwapa wake zake wawili penzi motomoto kwa miaka 30.
Alikuwa amewekewa mamba wengine wawili aishi nao lakini akawala.
David Mbatu, mmoja wa wahudumuwa Mamba Village wanaosaidia kuandaa harusi hiyo anasema keki ya harusi itakuwa ni mfupa wenye mnofu wa nyama na damu.
"Big Daddy alikuja hapa mwaka 1986 tukamchagulia wake wanne, akaua wake wawili akabaki na hawa wawili. Sasa amekuwa na hao wawili kwa miaka 30. Sasa kama ameonyesha upendo wa miaka hiyo basi tuonyeshe mfano pia mamba anaweza akafanyiwa ndoa," anasema.
Mipango ya awali ilikuwa harusi ifanyike mwezi Desemba lakini baadaye wakakumbuka kwamba kipindi hicho mamba huwa wana mayai.
"Hajajua. Atajua tu siku hiyo, kwa sababu tutafanya mazoezi kumuonyesha kwamba kuna kitu fulani kitakuja. Wajua mamba ana kumbukumbu nzuri sana."
Kwa vile hawawezi kuwavalisha mamba hao nguo za harusi, watajaribu kuwapamba.
Maimuna Siraj pia ni miongoni mwa wanaopanga harusi hiyo.
"Ukiangalia mapenzi yao yanavutia, mara wenyewe wanakumbatiana, wanapigana busu. Na ukiangalia ni sehemu moja. Kama ni mtu mwingine, angetengea nyumba mbalimbali au boma kando kando."
Makubwa haya

No comments:

Post a Comment