Thursday, September 22, 2016

TANZANIA KIDEDEA KWA AFYA NZURI DUNIANI

Watoto wa Tanzania wana afya nzuri ya maungo duniani

Watoto wa Tanzania wana afya nzuri ya maungo kuliko wenzao duniani
 Tanzania ndilo lenye watoto wenye afya nzuri ya maungo duniani, kulingana na utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Australia.
Viwango vya afya ya maungo ya watoto milioni 1.1 walio kati ya umri wa miaka tisa hadi 17 kutoka mataifa 50 vilifanyiwa ukaguzi.
Watoto hao walifanyiwa zoezi la kukimbia umbali wa mita 20,ambalo hukagua afya yao ya maungo.
Grant Tomkinson, mmoja ya watafiti wakuu wa chuo cha Kusini mwa Australia ameiambia BBC kwamba watoto wa Tanzania waliibuka washindi kutokana na utendaji wao.
BBC

No comments:

Post a Comment