Wednesday, September 14, 2016

DARAJA LA CHOTE KIJIJI CHA PINGONI HATARI TUPU



Wakazi wa kijiji cha Pingoni kata ya Pongwe Tanga wakipita kwa shida daraja la Chote ambalo kingo na mbao zimeibwa na watu wasiojulikana  na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa daraja hilo ambalo ndio njia pekee ya kuelekea ng’ambo ya pili. Daraja hilo ambalo lilijengwa na wakoloni linatumika hadi leo hii.
Daraja hilo lililojengwa na Wakoloni mwaka 1950 hadi leo limekuwa likitumika ila kuna baadhi ya watu ambao sio waaminifu wamekuwa wakikata vyuma na kuviuza kama chuma chakavu.
Hali hii imekuwa hatarishi hasa vipindi vya mvua kubwa ambao chini kuna mamba na kuhatarisha usalama wa wananfunzi waendapo shule na wapita njia pamoja na kuwa daraja hilo ndilo pekee la kupitia na kusafitrisha mazao pamoja na wafanyabiashara wa mkaa.









Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment