Thursday, September 29, 2016

CHAVITA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWEKA WATAALAMU WA LUGHA ZA ALAMA KWENYE LUNINGA



Tangakumekuchablog
Tanga, CHAMA Cha Viziwi Tanzania (Chavita) Kimeikumbusha Serikali kuwawekea wakalimani wa lugha za alama katika Televisheni ili kuweza kupata habari za Bunge na za kitaifa na Kimataifa na kuacha kusimuliwa.
Akizungumza katika Kongamano la Wajasiriamali Viziwi kuhusiana na kujiunga na Mifuko ya Bima, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa , Nibros Mlawa, amesema walemavu wa kusikia wamekuwa wahanga wa kukosa habari kwa  muda mrefu.
Ameliomba Bunge kupitisha sheria ya kila Televisheni kuweka mkalimani wa lugha za alama jambo ambalo litasaidia kupata na kujua matukio yanayojiri na kuepukana na kupata habari za kusimuliwa ambazo nyengine hazina ukweli.
Akikumbushia walemavu kujiunga na mifuko ya jamii, Mlawa amesema walemavu wako tayari kujiunga na mifuko hiyo lakini kwanza kuboresha miundombinu ya kuyafikia matibabu ikiwemo kuweka ngazi maalumu kwa walemavu na barabara.




Mwenyekiti wa Chama Cha Viziwi Tanzania (Chavita), Nibros Mlawa, akizungumza na waandishi wa habari Tanga jana mara baada ya kufungua warsha ya wajasiriamali viziwi kupata elimu ya kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya , kulia ni mkalimani kutoka kituo cha watoto wenye ulemavu (YDPC) Prisca Mwakasendile.


 Afisa Jinsia na Maendeleo Makao Makuu ya Chama Cha Viziwi Tanzania (Chavita), Lupi Mwaisaka, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa warsha ya Wajasiriamali Viziwi kupata elimu ya kujiunga na Bima ya Afya , kulia ni mkalimani wa kituo cha watoto walemavu (YDPC), Prisca Mwakasendile.
Kwa habari , matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment