Tuesday, September 13, 2016

MWANAMKE AJIFUNGUA KWENYE MAJI AKIOGELEA

Video ya mwanamke akijifungua mtoto akiwa kwenye maji imevuma sana mtandaoni baada yake kuonekana kujifungua kwa urahisi kuliko kawaida.
Wanawake wengi hutatizika sana wanapojifungua lakini kwa Audra Lynn inaonekana kuwa kama shughuli rahisi sana.
Video yake akijifungua katika eneo la Orange , California inashangaza kwa sababu mtoto anaonekana kutoka baada ya misuli yake kujikaza mara chache tu.
Video yake ambayo imepakiwa katika mitandao ya Instagram na Facebook, imetazamwa zaidi ya mara 16 milioni tangu ilipopakiwa Septemba 3.
Mkunga Lisa Marie Sanchez Oxenham ambaye alipiga video hiyo anasema lilikuwa "tukio la kushangaza".
Audra Lynn na mumewe Pete wakiwa na mtoto wao

No comments:

Post a Comment