Tuesday, September 13, 2016

VIWANJA 8 KUTIMUA VUMBI ULAYA LEO, ARSENAL YAIFUATA PSG

ligi ya mabingwa ulaya kuanza kutimua vumbi leo

Nembo ya ligi ya mabingwa
Michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya inaanza kutimua vumbi leo kwa jumla ya viwanja vinane kuwaka moto.
Katika kundi A miamba wa soka la Ufaransa, Paris St Germaine watakua nyumbani kuwaalika Arsenal toka England, huku Basel wakichuana na Ludo Razgrad.
Michezo ya kundi B Wareno wa Benfica watashuka katika dimba lao la Estádio da Luz kuwakabili Besiktas toka uturuki, Dynamo Kiev nao watapambana na Napoli.
Fc Barcelona watashuka dimbani Camp Nou kukipiga na Celtic,matajiri wa Manchester City wataanza kusaka heshima kwenye michuano hiyo kwa kucheza Wajerumani wa Borussia Monchengladbach.
Michezo ya kundi D Bayern Munich watakua nyumbani kucheza na Fc Rostov huku Waholanzi wa PSV Eindhoven wakicheza na Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment