Monday, September 26, 2016

SERIKALI KUPAMBANA NA WACHAFUZI WA MAZINGIRA BAHARINI

 Tangakumekuchablog


Tanga.Serikali inatarajia kuzindua mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa bahari  ikiwa ni njia ya kukabiliana na changamoto itakayotokana na ongezeko la meli kubwa zitakazokuwa zikitia nanga katika bandari za Tanzania bara na Zanzibar.

Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wan chi kavu na majini (Simatra),Captain Mussa Mandia alisema hayo leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia  maadhimisho ya wiki ya bahari duniani yanayofanyika kitaifa jijini Tanga.

Alisema Serikali ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa bahari (NMOSCRP) ambao utaviwezsha vyombo vinavyohusika na bahari kuhakikisha mazingira ya bahari hayachafuliwi.

“Serikali ya awamu ya tano imeazimia kuendesha uvuvi wa kisasa katika bahari ya hindi na maziwa yake kwa maana hiyo ni wazi kwamba zitakuja meli kubwa kuvua,kama hatutaweka mpango wa kudhibiti uchafuzi  bahari yetu itachafuliwa sana”alisema Mandia.

Alisema uzinduzi wa mpango huo utafanyika wiki hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya bahari dunia ambapo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzui na mawasilianoProfesa Makame Mbarawa atakuwa mgeni rasmi.

Selemani Musa Makame kutoka Mamlaka ya meli Zanzibar (ZMA),alisema katika uzinduzi huo,Waziri wa Biashara ,Amina Salum Ali  ataiwakilisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika uzinduzi huo.

                         MWISHO


 ,Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini  (Sumatra) Mussa Mandia, akizungumza na waandishi wa habari Tanga jana kuzungumzia mpango wa maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Devid Mzirai, Meneja Mawasiliano Sumatra.


 Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wan chi kavu na Majini (Sumatra) Mussa Mandia, akizungumza na waandishi wa habari jana kuzungumzia mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kulia ni Mkurigenzi Mkuu Mamlaka ua Usafiri Baharini Zanzibar, Suleiman Massoud.

 Waandishi wa habari wakichukua habari wakati w amkiutano wa waandishi wa habari leo



Mwandishi wa habari wa Radia Huruma ya Tanga, Pamela Chaullah akiwajibika wakati wa mkutano leo

No comments:

Post a Comment