Vyoo vilivyojengwa kwa vioo vyazinduliwa nchini China


China imezidisha
matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa kujenga choo cha
vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani.Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani.
Aidha, walio nje wanaweza kuona walio ndani ya vyoo
Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema ni watu wachache sana waliotumia vyoo hivyo siku ya kuzinduliwa kwake.
No comments:
Post a Comment