Wednesday, September 14, 2016

KERO YA MAJI YAHAMISHA FAMILIA MUHEZA


Tangakumekuchablog
Muheza, BAADHI ya familia kijiji cha Kirapula kata ya Ngomeni Muheza Tanga wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia kero ya maji ilichokikumba kijiji chao kwa muda mrefu.
Pia familia hizo wamesema ndoa zao huingia katika migogoro kwa kulazimika kuamka saa tisa usiku ili kuwahi foleni ya maji kwenye kisima kimoja ambacho maji yake hayana uhakika .
Wakizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo leo, familia hizo wamesema wamelazimika kuzihama nyumba zao kuepuka kuzuka kwa magonjwa ya miripuko ukiwemo wa matumbo na kichocho.
“Kero yetu hapa ni ya muda mrefu na viongozi wetu wanajua na tumekuwa tukipewa ahadi kila siku, kwa sasa subira imezidi na ni bora kujisalimisha kuepuka magonjwa” alisema Sofia Hassan na kuongeza
“Watoto wetu wamekuwa wakienda shule bila kuoga na nguo chafu jambo ambalo linawalazimu baada ya kutokuwa na njia mbadala ya kupata maji na hilo linarudisha nyumba uelewa wa masomo darasani” alisema
Kwa upande wake Diana Hassan, alisema kero hiyo ya maji imekuwa ikiwaingiza katika migogoro ya ndoa na waume zao baada ya kulazimika kuamka saa tisa usiku kuwahi foleni katika kisima kimoja kilichopo pekee.
Alisema baadhi ya siku husindikizwa na waume zao na siku nyengine waume hugoma kuamka jambo ambalo hupelekea kutoka peke yao hivyo unapochelewa kurejea hupatwa na maswali.
“Kero ya maji inatuingiza katika mizozo na waume zetu kwani unapochelewa unapatwa na maswali mengi huku ikieleweka  wazi kuwa hukumbana na foleni hata uamke saa nane usiku” a;lisema Diana
Nae Bakari Mauya, alisema hulazimika kuamka usiku wa saa kumi pamoja na familia yake na watoto na kila mmoja hubeba ndoo moja ambayo hutumia hadi siku ya pili.
Alisema hupata nafuu vipindi vya mvua kwa kuhifadhi katika mapipa na ndoo na kuepukana na adha ya utafutaji maji usiku na kusema kuwa endapo ukichelewa unaweza kukosa maji ya kutumia mchana mzima.
Alisema ili kuweza kuzinusuru afya na wakazi wa Kilapula na kubaki katika makazi yao Serikali kuweza kuwawekea kisima cha maji safi ambacho watakuwa na uhakika wa upataikanaji na kuepukana na adha ya kuamka usiku wa manane.
                                             Mwisho






No comments:

Post a Comment