Friday, September 23, 2016

BAH WA SIERRA LEONE AFARIKI KWA AJALI FREETOWN

Mwanasoka wa Sierra Leone, Bah afariki kwenye ajali

Mamadu Alphajor Bah (right)
Aliyekuwa mwanasoka wa kimataifa, raia wa Sierra Leone, Mamadu Alphajor Bah amefariki dunia katika ajali mbaya ya barabarani iliyofanyika karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Freetown.
Gari la mchezaji huyo wa kiungo kati aliye na umri wa miaka 39 liligongana na lori uso kwa uso wakati wa ajali hiyo.
Alikimbizwa hospitalini Goderich, lakini akafariki punde kutokana na kupoteza damu nyingi. Polisi wangali wanachunguza ajali hiyo.
Bah aliwahi kuichezea nchi yake Sierra Leone mara 25 katika mechi za kimataifa.
Mchezaji mashuhuri Mohamed Kallon, aliyekuwa nahodha wa timu hiyo wakati Bah alipokuwa angali anacheza, amelitaja tukio hilo kama pigo kuu.
Mchezaji mwenzake mwengine Ibrahim Kargbo,nae amesema : 'Ni kama ndoto mbaya , kweli nimeshtuka, ni kaka ambae daima atakuwa nasi kwenye fikira zetu, Mungu amweke mahala pema peponi ''.
Bah alisifika sana kama mmojawapo wa wachezaji bora wa timu ya taifa la Sierra Leone hasa katika miaka ya 2000 hadi 2008.
Katika ngazi ya klabu , aliichezea timu ya ubelgiji ya KSC Lokoren hapo 1994-96 kabla ya kuelekea Korea kusini kuichezea Chunnam Dragons hapo 1997.
Miaka miwili baadae alielekea UChina na kuwa raia wa kwanza wa Sierra Leone kucheza katika ligi kuu itwayo Chinese Super league, akiwa katika klabu ya Xiamen Lanshi mwaka wa 1999-2003 kisha akahamia klabu ya Zhejiang Lucheng hapo 2004.
Pia aliwahi kuchezea klabu ya Halmstad BK huko Sweden

No comments:

Post a Comment