Tuesday, October 18, 2016

CHINA YAONGOZA KWA UCHANGIAJI WA VIUNGO VYA BIANADAMU DUNIANI

China yaongoza kwa uchangiaji wa viungo vya binadamu duniani..

October 18 2016, Mtu wako wa nguvu nimeipata ripoti hii kutoka mkutano wa kimataifa wa uchangiaji viungo vya binadamu wa mwaka 2016 ambapo imeelezwa kuwa hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2016 watu 8,866 wa China walichangia viungo elfu 25 baada ya kufariki, na idadi ya viungo vilivyochangiwa katika robo tatu ya mwanzo ya mwaka huu imeongezeka kwa nusu kuliko mwaka jana kipindi kama hiki.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkutano wa kimataifa wa uchangiaji na upandikizaji wa viungo kufanyika nchini China, imeelezwa kuwa hali hiyo inatokana na maendeleo ya kasi ya uchangiaji na upandikizaji wa viungo na kuendelea kukamilika kwa mifumo husika katika miaka kadhaa iliyopita.
Taarifa ya Mkurugenzi wa kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China Li Bin imesema, China imejenga kwa hatua ya mwanzo mfumo wa uchangiaji na upandikizaji wa viungo vya binadamu ambao unafuata kanuni za kisayansi na maadili ya kibinadamu, na pia unalingana na hali halisi na utamaduni wa China.
>>>China imekamilisha mfumo wa uchangiaji na ugavi wa viungo vya binadamu, sasa imetimiza utaratibu wa kugawa viungo kulingana na mahitaji kwa njia ya kompyuta, na vilevile China imeanzisha njia maalumu za kusafirishia viungo ili kupunguza muda wa kuvifikisha kwa wenye mahitaji na kuokoa maisha yao.
Aidha, China pia imejenga mtandao wa usimamizi wa viungo, ili kuweza kuvifuatilia na kuvisimamia wakati wote. Haswa katika mwaka 2015, China imefanikiwa kuendeleza mageuzi kwa vyanzo vya viungo vya binadamu, ambayo ni mafanikio ya kihistoria:- Li Bin
Ripoti kutoka mkutano huo zinasema kuanzia Januari 1, 2016 China imeacha kabisa kutumia viungo vya wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo ili kufanya upandikizaji na uchangiaji wa hiari wa viungo vya binadamu baada ya kufariki.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Bi. Margaret Chan amepongeza mafanikio yaliyopatikana nchini China katika upandikizaji wa viungo, Katibu huyo amesema China imetekeleza mageuzi kwa mwelekeo sahihi na kwa ufanisi, na Shirika la afya duniani litaendelea kuunga mkono kazi za uchangiaji na upandikizaji wa viungo nchini China.
millardayo

No comments:

Post a Comment