Monday, October 17, 2016

MSHUMAA WATEKETEZA NYUMBA MTAA WA BOMBO TANGA

 Askari wa Kikosi Cha  Zima moto na Uokozi Tanga wakizima moto katika nyumba mtaa wa Bombo Tanga iliyoungua na mashuhuda wamedai kuwa chanzo ni mshumaa kuunguza kipande cha ngua kisha kushika kasi na kutambaa chumbani.
Wakielezea tukio hilo na kuiambia tangakumekuchablog watoto wawili ambao walikuwemo ndani ya nyumba hiyo wakati mzazi wao akiwa kanisani.
Wamedai kuona moshi mkubwa ukiwa umetanda kisha kuzuka moto ambao uliunguza thamani za ndani na kutekekeza kila kitu.
Kwa jitihada za Kikosi cha Zima moto na Uokozi walifanikiwa kuuzima lakini chumba kimoja kiliteketea na kuunguza kila kitu.





 Wakazi wa Bombo Erea Raskazone Tanga wakiongozwa na mwenyekiti wa mtaa  wakiangalia mabaki ya thamani za ndani baada ya kuzuka moto na kuteketeza vitu mbalimbali ambavyo thamani yake haijajulikana.



No comments:

Post a Comment